Sizwe Mankazana (pichani), dereva wa gari iliyohusika na ajali iliyomuua kitukuu wa rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, ameachiliwa baada ya kesi yake kutupiliwa mbali na mahakama.
Alikuwa anamrejesha nyumbani Zenani Mandela kutoka kwenye tamasha la kabla ya kuanza kwa kombe la dunia mwaka 2010, wakati gari lililokuwa limewabeba lilipogonga chuma.
Wakili wa Sizwe amesema kuwa mteja wake amefutiwa madai yote dhidi yake ikiwemo kuendesha gari akiwa mlevi.
Zenani alikuwa mmoja wa vitukuu tisa wa Mzee Mandela.
Afrika Kusini ina mojawapo ya rekodi mbaya sana za usalama wa barabarabni na inakadiriwa kuwa watu 42 hufariki kila siku katika barabara za nchini humo.