Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Takukuru yaahidi kuwachunguza maofisa Tanapa

 

 

Mkurugenzi Takukuru,Dk Hosea
   
MKURUGENZI wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah amesema taasisi hiyo haitasita kuwachunguza wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), wanaodaiwa kuwanyanyasa wawekezaji wa Kampuni ya Kitalii ya Ahsante Tours.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuiandikia barua ofisi ya Takukuru akiitaka kufanya uchunguzi dhidi ya watendaji hao wa Tanapa.
Taarifa zilizolifikia Mwananchi jana zilieleza kuwa tayari barua hiyo imeshafika Takukuru na taratibu za uchunguzi zimeanza kufanyika.
Sakata hilo liliibuka baada ya kudaiwa kuwa uongozi wa Tanapa umeifungia kampuni hiyo kuwatembeza watalii katika hifadhi mbalimbali bila kulipa ada inayofikia Dola 80,000 za Marekani sawa na Sh155 milioni ilizoikopesha.
Inadaiwa kuwa baada uamuzi wa Tanapa kuifungia kampuni hiyo kutembeza wageni katika hifadhi zote nchini kutokana na kashfa hiyo, kampuni hiyo ililalamika kwa Waziri Nyalandu, ambaye aliamuru Tanapa wakae pamoja na kampuni hiyo,ili kuweza kuwezesha urejeshaji wa pesa hizo.
Hata hivyo, Nyalandu alikanusha kuingilia utendaji wa Tanapa, akisema kuwa hakukurupuka katika kufanya uamuzi huo na kwamba alifanya hivyo baada ya kubaini Tanapa ilifanya makosa kuikopesha kampuni hiyo kinyume na taratibu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Hoseah hakutaka kuzungumzia suala hilo kiundani huku akifafanua kwamba hakuwepo ofisini lakini kuna uwezekano mkubwa barua hiyo ikawa imeshafika ofisini kwake. “Nilikuwa safari ila kuna uwezekano barua hiyo ikawa imefika ofisini kwangu,” alisema Dk Hoseah.
Alipoulizwa kama taratibu zinazofanywa na Takukuru baada ya kupewa maelezo ya kuwepo kwa mianya ya rushwa, alisema alitaka kupewa muda ili kujiridhisha kama barua hiyo ipo, kueleza taratibu za kuanza kwa uchunguzi huo.
Katika maelezo yake Nyalandu alisema, baada ya kupokea malalamiko ya Ahsante Tours yanayoashiria kuwa uamuzi wa kufungiwa na Tanapa siyo tu ungeathiri wafanyakazi wa kampuni hiyo, bali kodi za Serikali pamoja na watalii wanaokuja nchini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top