Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAELFU WAMZIKA ZOLA WA YANGA JIONI YA LEO KISUTU

 



Mwili wa marehemu Hamza Said 'Zola' (katika picha ndogo) ukiwasili makao makuu ya klabu kwa ajili ya kuangwa na wapenzi wa soka, washabiki na wanachama kabla ya kupelekwa katika makaburi ya Kisuru kwa mazishi leo.
Na Mwandishi Wetu
MAMIA ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa soka leo jioni wameshiriki katika safari ya mwisho ya kuusindikiza mwili wa aliyekuwa mfanyakazi wa klabu ya Yanga, marehemu Hamza Said ‘Zola’, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana mjini Dar es Salaam, ambaye amezikwa katika makaburi ya Kisutu, Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga akiweka
mchanga katika kaburi la marehemu Hamza Zola

Mazishi ya Zola yaliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, Wenyekiti wa zamani wa klabu, Mzee Dk. Jabir Idrisa Katundu, na Wakili Iman Omar Madega na viongozi wengine mbalimbali waliowahi kuongoza klabu hiyo ya kihistoria nchini.
Marehemu Zola ambaye alifikwa na umauti jana alfajiri katika makutano ya mitaa ya Rufiji na Kongo kwa ajali ya kugongwa na gari, alikua akitokea mitaa ya Kariakoo akitembea kuelekea makao makuu ya klabu na ndipo gari hilo lilipomgonga kwa nyuma wakati akitembea kuelekea klabuni.
Uongozi unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na wapenzi wa soka nchini kwa kuondokewa na rafiki yetu kipenzi.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen
 
Imechotwa: Bin Zubeiry
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top