Picha na Maktaba.
Na Jennifer Chamila-MAELEZO
KIJANA
wa Kitanzania Hamisi Kondo aibuka mshindi wa dunia katika mashindano ya
kuruka kamba yaliyo fanyika Orland Marekani Julia 5 hadi Julai 13 mwaka
huu.
Mashindano
hayo yalihusisha nchi kumi na nne zikiwa na wachezaji 480 huku Bara la
Afrika likiwakilishwa na Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini
ambapo kijana Hamisi mwenye umri wa miaka 14 Mtanzania aliweza kujinyakulia ushindi huo.
Kijana
huyo ambaye ni yatima aliyelelewa na kituo cha
kulelea watoto yatima cha Dogodogo Center kilichopo jijini Dar es
Salaam na kupata mafunzo ya mchezo wa kuruka kamba kituoni hapo na
baadae kupata ufadhili kutoka kwa Bwana na Bibi Amy Canady nchini
Marekani ambako aliweza kusoma na kuendeleza kipaji chake.
Akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Hamisi amezungumzia
mafanikio yake na kuwaasa vijana wenzake kutokata tamaa ya maisha kwa
kuwa na juhudi ya kupambana ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
“Nawaomba
watoto wa mtaani na yatima kutokata tamaa ya maisha kwani hata mimi
nilikuwa kama wao na nimeweza kufanya juhudi na kufanikiwa”alisema
Hamisi.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo
,kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana
Yassoda aliwaomba vijana kutong’ang’ania michezo mikubwa kama mpira wa
miguu kwani kuna michezo midogo midogo ambayo wanaweza kucheza na
kufanikiwa kama ilivyo kuwa kwa Hamisi.
Pia
Mwenyekiti wa Kituo cha Kufundisha Michezo Tanzania (TSTC), Bw.Dennis
Makoi ambaye alishirikiana na kituo cha dogodogo kumtafutia ufadhili
Hamisi nchini Marekani,ametoa shukrani zake za dhati kwa familia ya Bw.
na Bi.Amy Canady wa huko Marekana kwa ufadhili na kusaidia kufanikisha
ushindi huo.
Hivi sasa Hamisi anaendelea na masomo nchini Marekani.
Post a Comment