Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Unyonyeshaji maziwa ya mama wapungua nchini


UNYONYESHAJI maziwa ya mama umepungua katika jamii za Watanzania, kutokana na mmomonyoko wa maadili unaoendelea katika nyanja mbalimbali na kusababisha udumavu wa watoto kwa asilimia kubwa. Akizungumza Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, alisema maziwa ya mama ni kinga kwa mtoto.

Alisema dhana zinazojengeka katika jamii ni ulishaji watoto kwa kutumia maziwa mbadala ya kopo na nyonyo bandia za kulishia watoto kuwa ndiyo bora zaidi kuliko kunyonyesha maziwa ya mama, hali inayowaletea watoto madhara ya kukosa baadhi ya virutubishi.

“Athari za ulishaji mbadala ni pamoja na kuchangia katika ongezeko la maradhi ya kuhara, maradhi ya mfumo wa kupumua, mzio na tatizo la watoto kuwa na uzito uliozidi na kiriba tumbo.

“Taratibu za unyonyeshaji zinazotekelezwa hazikidhi viwango vya ubora unaopendekezwa na wataalamu wa afya na ulishaji watoto na hivyo kusababisha matatizo mbalimbali,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema asilimia 50 ya watoto ndiyo wanaoanzishiwa vyakula vya nyongeza katika umri sahihi wa miezi sita unaopendekezwa na wataalamu wa afya huku asilimia 21 ya wanawake ndio huendelea kunyonyesha watoto wao hadi kufikia umri wa miaka miwili.

Alisema matokeo ya taratibu za unyonyeshaji zisizokidhi viwango, zimechangia Tanzania kuwa ya tatu baada ya Ethiopia na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC), katika Bara la Afrika, ni kwa kuwa na viwango vikubwa kwa asilimia 42.


MTANZANIA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top