Katika
ziara hiyo Waziri Lukuvi amewaagiza Wakala wa Hifadhi ya Chakula NFRA
pamoja na TRL kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuanza kusafirisha
Mahindi mapema kuelekea Shinyaga kabla ya kuanza kwa mvua ili kuweza
kupunguza gharama za usafirishaji katika kipindi hicho, alisema hayo
tarehe 17 Septemba, 2013. Habari Picha na Afisa Habari Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya WaziriMkuu Sera, Uratibu na Bunge,
Mhe. William V. Lukuvi (MB)akipokea maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa
Kituo cha Mpanda Bw. Nahoda Khatib (wakatikati)wakati wa Ziara yake kikazi
katika Mkoa wa Katavi iliyoanza jana tarehe 16 Septemba,2013. Kushoto
(mwenyetai) ni Bw. C. Sadda Meneja Usafirishaji Kanda ya Tabora.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. William V.
Lukuvi (MB) akikagua Soko la Kimatifa la Mahindi la Isunta katika Wilaya
ya Nkasi akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea sehemu za
Ununuzi na Uhifadhi Mahindi nchini.



Post a Comment