Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

OFISI YA TENDWA YAWATUPIA KOMBORA CHADEMA


OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakina ubavu wa kumkataa au kutomtambua John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasai, Rajab Baraka alipozungumza na MTANZANIA kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa aliyedai chama hicho hakimtambui John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa.

Katika madai yake Dk. Slaa alidai Tendwa anakipendelea CCM katika kutoa haki ya demokrasia na hatendi haki kama mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini.

Dk. Slaa alisema hayo wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari na kusisitiza hata katika barua zao za mawasiliano kwenda kwa ofisi ya msajili chama hicho hakitumii jina la John Tendwa.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Chadema kinaitambua ofisi ya Msajili wa Vyama tu lakini hakimtambui Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

“Hatumpelekei hata barua huyu hatunzi sheria siyo mtu wa kulea vyama ni mlezi wa chama kimoja, hayuko serious na hatushirikiani naye mpaka aondoke madarakani.

“Tukiandika barua hatuweki jina lake lakini tunaitambua ofisi yake, hata yeye mwenyewe analijua hilo na akijibu barua zetu haweki jina lake,” alidai Dk. Slaa.

TAARIFA SAHIHI DHIDI YA UVUMI KUHUSU WANAFUNZI WANAOENDELEA KULAZIMIKA KUJAZA TENA TAARIFA ZAO ZA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

 

2704heslbKumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.
Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.
Aidha Bodi inasisitiza  kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.
Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz
Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Askari kituo cha Osterbay wakamatwa na meno ya tembo 70

 

WATU tisa, wawili kati yao wakiwa ni askari wa Jeshi la Polisi kituo cha Osterbay jijini Dar esalaam wamekamatwa wilayani Kisarawe Mkoani Pwani kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha meno ya tembo (ndovu) 70 sawa na kilo 305 kinyume na sheria. Meno hayo ya tembo kwa mahesabu ya kawaida ni sawa na Tembo 35 ndiyo wameuawa na kwamba thamani ya meno hayo ni  zaidi ya sh, milioni 850 fedha za kitanzania.


Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Ulrich Matei amesema watuhumiwa haobwamekamatwa saa 5.30 usiku wa Julai 28 huko Kisarawe na Askari Polisi na maliasili wilayani humo waliokuwa kwenye operesheni ya kukamata pembe za ndovu.

Matei amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika kizuizi cha Kauzen kata ya Vikumbulu tarafa ya Chole ambapo walikuwa wakisafirisha meno hayo kwa kutumia gari T 357 ABK Toyota Surf kutoka wilayani humo kwenda jijini Dar esalaam.

Kamanda huyo wa Polisi Pwani amewataja watuhumiwa hao ni Hamidu  Hamadi wa Tandika Yombo, Musa Muhamed Ali wa Kinondoni Studio, Prospa Maleto mkazi wa Tandika hewa, Amir Bakar mkazi wa Mbagala Chalambe,Seif Mdumuka, Said Kadro na Ramadhan Athumani  wa Chanika.

Matei amewataja pia askari Polisi  wawili waliokamatwa pia kuwa ni Koplo Senga Idd Nyembo na PC Issa Mtama ambao wote wanadaiwa ni watumishi wa Jeshi la Polisi kituo cha Ostabay  jijini Dar esalaam na wanatarajiwa kutolewa Kisarawe walikokamatiwa na kufikishwa Kibaha makao makuu wa jeshi hilo mkoani Pwani kwa ajili ya hatua zingine za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Chanzo: tabianchi

Diwani wa Chadema aomba kura kwa kuinadi CCM


DIWANI mmoja wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyekuwa anagombea umakamu mwenyekiti wa halmashauri ya Geita, aliomba kura kwa kunadi sera za Chama cha Mapinduzi(CCM), imefahamika. Diwani huyo, Dioniz Bugali wa Kata ya Kamhanga, vilevile alimteua Diwani wa CCM kuhesabu kura zake.

Bugali alifanya kituko hicho mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Geita kwenye mkutano wa nne wa baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Katika uchaguzi huo wa makamu mwenyekiti wa halmashauri, mgombea wa wa CCM alikuwa Masoud Kimondo ambaye ni diwani wa kata ya Kaseme na kwa Chadema alikuwa yeyé, Bugali.

“Nimesimama hapa kuomba kura…kabla ya kuomba kura naomba niseme neno…nafasi hii ya makamu mwenyekiti wa halmashauri sikuwa naitaka isipokuwa nimelazimishwa na chama changu(CHADEMA)kugombea.

“Nachotaka kusema hapa ni kwamba nikishindwa sitakata rufaa.

“Ninampongeza sana mgombea mwenzangu wa CCM,mimi hapa pamoja na kuwa ni diwani wa Chadema na ninagombea nafasi hii kupitia chadema,lakini bado ni katibu mwenezi wa CCM kwenye kata yangu ya Kamhanga…nipeni kura zenu,”alijinadi Dionizi baada ya kupewa nafasi kuomba kura.

Kauli hiyo ilisababisha madiwani wa CCM kulipuka kwakicheko wakidai Bugali ni mwenzao na wengine wakiitambia Chadema kwa kusema, “Haloohalooooooooooooooo … Chadema mmesikiaaaa…hiyo ndiyo CCM…Spidi 120…Chadema hamna chenu Kamhanga huyo ni mwenzetu.”

Mahojiano na waTanzania wanaomiliki Chuo cha Uuguzi Kansas City nchini Marekani

 


Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Kansas College of Nursing wakiwa darasani


Wafanyakazi wa Kansas College of Nursing

Wanafunzi wa Kansas College of Nursing

Wanafunzi wa Kansas College of Nursing


Karibu katika mahojiano baina ya Jamii Production na waTanzania wanaomiliki Chuo cha Uuguzi cha Kansas Ndg Michael Katunzi na Ndg Robert Otto.

Katika mahojiano haya, wanaeleza mambo mbalimbali ikiwemo walipopata na walivyopata wazo la kuanzisha chuo hiki, walivyoanzisha na walipo hivi sasa, changamoto walizokutana nazo kuanzia kuanzisha mpaka kilipo sasa, mafanikio yao na ya chuo chao pamoja na mipango yao juu ya chuo hicho kilicho katika nafasi za juu miongoni mwa vyuo vya uuguzi jimboni humo.

Karibu uungane nasi


SIMBA DAY YASOGEZWA MBELE

Na Mahmoud Zubeiry, wa Bin Zubeiry
 
TAMASHA la kuazimisha siku ya Simba SC linaweza kusogezwa mbele kwa simu mbili, kupisha sikukuu ya Eid El Fitri hivyo kufanyika Agosti 10, badala ya Agosti 8, kama ilivyo kawaida yake.
Aidha, mpango wa Simba SC kucheza na mabingwa wa Afrika mara nne, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umeshindikana kutokana na timu hiyo ya Lubumbashi kutingwa na michuano ya Kombe la Shirikisho.
Simba SC

Na kwa sababu hiyo, timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam sasa itacheza na SC Villa ya Uganda katika tamasha hilo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba ilitumai kucheza na Mazembe yenye wachezaji wake wa zamani wawili, Mbwana Samatta na Patrick Ochan ambao iliwauzua klabu hiyo miaka miwili iliyopita, lakini ratiba ya michuano ya CAF imeharibu mambo. 
Katika maendeleo mengine, wachezaji wa Simba SC waliokuwa na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wanatarajiwa kujiunga na wenzao kambini, Bamba Beach, Kigamboni kuanzia leo jioni.
Wachezaji waliokuwa Stars ni viungo Amri Kiemba na Haroun Chanongo. Kiemba alicheza dakika zote 90 na kufunga la Stars ikilala 3-1 Uwanja wa Mandela, Namboole na kutolewa jumla ya mabao 4-1, baada ya awali kufungwa 1-0 Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, wakati Chanongo aliingia uwanjani dakika ya 78 kumpokea John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC.    

Kikwete aingilia kati ugomvi wa Kagasheki, Meya

 


 
Rais Jakaya Kikwete ameingilia kati ugomvi uliopo kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kaghasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatoli Amani, kwa kuwataka wakae chini na kumaliza tofauti zao kwani hakuna lisilokuwa na mwisho.

Rais aliyasema hayo katika uwanja wa Kaitaba alipokuwa akihitimisha ziara yake mkoani Kagera aliyoanza Jumatano wiki iliyopita.

“Mbunge na Meya wakiendelea kutiliana shaka wanaoumizwa ni wananchi, malizeni tofauti zenu kwa sababu hakuna lisilokuwa na mwisho,” alisema.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema masuala yaliyokuwa yakiwagonganisha Meya na Balozi Kaghasheki ambaye ni Mbunge wa Bukoba Mjini, ya ujenzi wa soko pamoja na viwanja ni mambo ya maendeleo.

Katika ugomvi huo, Kaghasheki anapinga ujenzi wa soko jipya mjini Bukoba kwa madai kwamba haukufuata maamuzi ya vikao vya Baraza la Madiwani wakati Meya akisisitiza ujenzi huo kwa maelezo kwamba maamuzi ya ujenzi yamepitishwa kwenye vikao vya baraza la madiwani.

Rais Kikwete alisema ujenzi wa soko ni suala la maendeleo lakini akataka Manispaa iwatafutie eneo wajasiriamali wanaoendesha biashara zao kwenye soko la sasa ambalo litavunjwa na kujengwa jipya.
Rais Kikwete aliagiza kuwa baada ya ujenzi, wananchi wanaondesha biashara zao katika soko hilo wapewe kipaumbele.

“Ujenzi wa soko ni maendeleo na karne hii ni ya teknolojia, ni uamuzi mwema; mkitaka mambo ya zamani basi na nyinyi mtakuwa ni watu wa kizamani,” alisema.

“Katika mradi huu mpya wa viwanja 5,000 kwanza wapeni hao 800 wa zamani maana walikwishalipia hilo ni deni la manispaa wala haliwezi kukwepeka hata kama viongozi wa sasa hawakuwapo wakati huo,” alisema Rais Kikwete.


HIVI HAPA VIWANGO VIPYA VYA MISHAHARA YA WATUMISHI WA SERIKALI 2013.

 


TGOS A
TGOS A 1. (Sh240,000), TGOS A 2. (Sh245,600), TGOS A 3. (Sh251,200), TGOS A 4. (Sh256,800), TGOS A 5. (Sh262,400), TGOS A 6. (Sh268,000), TGOS A 7.(Sh272,000), TGOS A 8(Sh279,000), TGOS A 9.(Sh284,800), TGOS A 10(Sh290,400), TGOS A 11(Sh296,000), TGOS A 12(Sh301,600), TGOS A 13(Sh 307,200), TGOS A 14(Sh312,800), TGOS A 15(Sh 318,400), TGOS A 16(Sh324,000), TGOS A 17(Sh329,600) na TGOS A 18(Sh335,200).
TGOS B
TGOS B 1. (Sh347,000), TGOS B 2. (Sh356,500) TGOS B 3 . (Sh366,000), TGOS B 4 . (Sh375,500), TGOS B 5. (Sh385,000), TGOS B 6. (Sh394,500), TGOS B 7. (Sh404,000), TGOS B 8. (Sh413,500), TGOS B 9. (Sh423,000), TGOS B 10. (Sh432,500), TGOS B 11 . (Sh442,000) na TGOS B 12. (Sh451,500).
TGOS C
TGOS C 1 . (Sh471,000), TGOS C 2 . (Sh482,000), TGOS C 3 . (Sh493,000), TGOS C 4. (Sh504,000), TGOS C 5. (Sh515,000), TGOS C 6. (Sh526,000), TGOS C 7. (Sh537,000), TGOS C 8. (Sh548,000), TGOS C 9. (Sh559,000), TGOS C 10. (Sh570,000), TGOS C 11. (Sh581,000) na TGOS C 12. (Sh592,000).

HII HAPA FULL VIDEO YA KADA NA KIONGOZI WA CHADEMA ALIVYOANIKA MAUCHAFU YAKE, ALIVYOMWAGA MITUSI YAKE MBELE YA MTOTO .... NI AIBU TUPU

 
 
"Mimi nimefanya wema, wema wangu umeniponza, wema wangu my assssss, wema wangu my fangasi....msenge we.
"Una wema wewe?? Ungekuwa na wema ungekuja kushika KU**********m ya dada ako wewe??....mshamba mkubwa, huna adabu". Alisema dada huyo
 


WAANDISHI WANYAKUA TUZO YA USALAMA WA BARABARANI

 

Na Jennifer Chamila,MAELEZO.TAASISI ya Automobile Association Tanzania (AAT) imetoa tuzo kwa waandishi wa habari kutoka katika  vyombo vya mbalimbali vya habari walio shiriki katika kutoa habari kwa wananchi kuhusu mafunzo yalio tolewa kwa waendesha bajaji na pikipiki  2500 kuhusu matumizi salama ya barabara.

Tuzo hizo zimetolewa leo  pamoja fedha taslimu na Rais wa taasisi hiyo Bw.Nizar Jivan katika sherehe fupi ilio fanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam,Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wamewaza kujinyakulia tuzo hizo.

 Rais  huyo alitoa tuzo  hizo  kwa waandishi na watu waliosaidia kukamilisha mafunzo hayo, ambapo    miongoni mwao ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw.Assa Mwambene, ambaye tuzo yake ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo, Zamaradi  Kawawa. 

Wengine waliopata tuzo hizo ni Mohamed Ugassa kutoka gazeti la The Guardian,Freginia Ole Swai kutoka ITV,Fred Mwanjara wa Channel Ten,Elias Shamt wa TBC,Miguel Suleiman wa Citizen,Nasongelya Kilyanga wa Daily News,Khadija Mussa wa gazeti wa Uhuru,Zainabu Malongo kutoka Mwananchi,Hadja Hamis kutoka Mtanzania,Abas Yusuph mwandishi wa kujitegemea,Judica Benedict wa The Guardian.

Akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe hiyo Bw.Nizar amesema kuwa,anawashukuru waandishi wa habari kwa kusaidia kutoa habari kwa wananchi juu ya mafunzo hayo yalio husisha matumizi salama ya barabara na jinsi ya kuepusha ajali za barabarani.

Vilevile taasisi hiyo imeitaka Serikali kuweka mikakati madhubuti ambayo itarahisisha kupambana na matumizi mabaya ya barabara.

“Serikali ihakikishe bodaboda zote zipewe namba maalumu ili iwe rahisi huzitambua pindi uhalifu utakapotokea kama ilivyo kwa teksi,” alisema Jivan.

MANJI AANIKA MKATABA WA YANGA HADHARANI

YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
“HIVI karibuni, Tanzania Football Federation (TFF)  iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina  mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:

Watata; Viongozi wa Yanga SC, kutoka kulia Balozi Ammy Mpungwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini, Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji, Waziri George Mkuchika, Mwenyekiti Baraza la Wadhamini, Francis Kifukwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini na Clement Sanga, Makamu Mwenyekiti wa klabu . 

1. BODI YA TPL
1.1 Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe  ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.

2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA
2.1 Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani. 

HAPA NDIPO MUUNGANO ULIPOZALIWA

Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) akibadilishana nyaraka na Mzee Abeid Amani Karume

MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa.

 

Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe Afungwa miaka 30
Hapa akijifunika sipigwe picha baada ya hukumu
Kulia ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake wakitoka mahakamani kulia ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na kuzalishwa

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 30, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC 0007 c7b85

BOFYA "Read More" HAPO CHINI KUYASOMA MAGAZETI YOTE KIUKAMILIFU

HII HAPA BARUA INAYOWAANIKA VIGOGO WAUZA MADAWA YA KULEVYA NCHINI .... LIST NI NDEFU MNO



Ni jambo la wazi wamba biashara ya madawa ya kuleya ni biashara ambayo mara nyingi hubebwa na watu wenye nazo au wenye madaraka fulani makubwa.Ni biashara ambayo ina faida kubwa na ya haraka pengine kupita aina nyingine yeyote ya biashara (halali na haramu).

Na kutokana na nguvu ya vyombo mbalimbali vya dola ulimwenguni katika kupambana na biashara hii, ni wazi kwamba bila kuwepo na connection za hali ya juu,utekelezaji wa biashara hii ungekuwa mgumu sana…

Ndio maana vita dhidi ya biashara hii haramu ni ngumu na ambayo inahitaji umakini wa hali ya juu zaidi katika kukabiliana nayo endapo kuna nia ya dhati ya kuitokomeza au japo kuipunguza.

Hivyo basi,haishangazi sana (japokuwa hizi ni tuhuma tu) kusikia yale yaliyotajwa katika “barua kutoka Hong Kong” kwa miongoni mwa watanzania wanaosemekana kufikia hata 200 wanaosota katika jela za nchini humo kusikia majina ya watu waliotajwa katika waraka huo ambao bila shaka utapamba vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wiki kadhaa zijazo.


Kutajwa kwa wazi wazi kwa majina ya baadhi ya wanaotuhumiwa kuhusika na huku mwandishi wa barua hiyo akionya kwamba majina mengine zaidi yapo, kunaifanya barua hiyo kuwa tofauti kabisa na barua za kawaida au hata zile tambo za kisiasa kwamba “wanaohusika na biashara hii nawajua”

Miongoni mwa majina hayo, limo jina la Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM,Iddi Azan.

Barua hiyo (ambayo utaisoma hapa chini) inahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina. Lakini kutokana na ukweli kwamba imeainisha watu wanaosadikiwa kuhusika, bila shaka imelipa jeshi la polisi mahali pazuri pa kuanzia. Je,wanaotajwa kipato chao kinatokana na biashara gani zilizo halali? Ukaguzi wa vitabu vyao vya fedha unasemaje?


Jambo moja ambalo linasikitisha sana (endapo tuhuma hizi zitathibitishwa hususani kumhusu Iddi Azan) ni kwamba Jimbo au Wilaya ya Kinondoni ni miongoni mwa maeneo ambayo yanaongoza kwa vijana kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya. Je, ina maana Mbunge wake anahusika katika kuangamiza vijana au wapiga kura wa jimbo lake mwenyewe?


SOMA BARUA YENYEWE HAPA CHINI…

MHE. PANDU KIFICHO ALITAHADHARISHA BARAZA LA WAWAKILISHI KUWA MAKINI KUFANYA MAAMUZI YAKE


mr-pandu-ameir-kifichoNa Ali Issa-Maelezo Zanzibar 
Spika wa baraza la wakilishi Zanzibar Pandu ameir kificho amesema Baraza la wakilishi liwe na Tahadhari sana kufanya maamuzi ambayo utekelezaji wake umo katika mikono ya Serikali ili kuiepusha Serikali kuja kuingia katika kitahanani kwa lile amblo kulitimizia Taifa mahitaji yake muhimu.
Hayo ameyasema  leo huko Baraza la wakilishi  wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa Kwamtipura CCM  Hamza Hassan Juma wakati alipokuwa amezuia kifungu kuipitisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kusema uagiziaji wa kuku kutoka Nnje uzuuliwe kwani una uwasokosesha mapato wafugaji wa ndani na kuliua soko lao.
Amesema si vyema kutoa maamuzi ya moja kwa moja kulilazimisha hilo kuzuia kuku kutoka nje wasiletwe nchini bila ya kuwa na utafiti wa
kutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.
 “sivizuri kuzuia fungu hili na kukusema kuku wasiagiziwe kutoka nje bali tuwachie Serikali wakachunguze ukweli wa hilo na baadae watuleteeripoti,”alisema Spika.
Aidha ali sema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina wapenda sana wananchi wake kuona kua wanafanikiwa katika uzalishaji kwani ndio
lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato wawe makini kuliko kuchukuwa maamuzi ya haraka.

ZITTO KABWE ATOA ANGALIZO .... HUU HAPA USHAHIDI WA TWEETS ZAKE ZA ANGALIZO ALIZOZIANIKA ...



1 
2


3

TAARIFA UJIO WA WAZIRI MKUU WA THAILAND NCHINI

 


Ndugu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,

Napenda nichukue fursa hii kuwajulisha rasmi kwamba Nchi yetu imepata heshima ya kutembelewa na Waziri Mkuu wa Thailand ambaye atawasili Nchini tarehe 30/07/2013.  Ziara hii ni ya kikazi (state visit) na atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere majira ya saa 6:30 mchana na kulakiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais wetu mpendwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa.



Ndugu Wananchi,

Baada ya kuwasili Mhe. Waziri Mkuu wa Thailand atakagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na pia atapata fursa ya kukagua vikundi mbalimbali vya ngoma ambavyo vitakuwa vikitumbuiza na kutoa burudani kwa Mgeni wetu na msafara wake.

Ndugu Wananchi,

Mgeni wetu baada ya kukagua vikundi vya ngoma na burudani ataondoka kuelekea Ikulu kupitia barabara ya Nyerere, Railway, Gerezani, Sokoine Drive hadi Ikulu. Akiwa Ikulu atasaini mikataba mbalimbali kati ya Serikali ya Tanzania na Thailand. Usiku atashiriki katika dhifa maalumu iliyoandaliwa na Mwenyeji wake.



Ndugu Wananchi,

Tunaomba radhi kwamba barabara hizi nilizozitaja zitafungwa kwa muda kupisha misafara ya Viongozi wetu Wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Kumbukumbu ya  Mwalimu J. K. Nyerere kumlaki Mgeni wetu hususan barabara ya Nyerere kuanzia saa 6.00 mchana hadi saa 7.30 mchana.



Ndugu Wananchi,

Tarehe 31/07/2013 Waziri Mkuu wa Thailand atatembelea Mbuga za Wanyama za Serengeti.Tarehe 01/08/2013 atarejea Dar es Salaam na kuagwa rasmi katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere na kuendelea na ziara yake huko Uganda.



Ndugu Wananchi,

Kama ilivyo ada tunaombwa kumlaki mgeni wetu kwa shangwe na bashasha katika maeneo yote atakayopita.

Asanteni kwa kunisikiliza.



     Saidi Meck Sadiki

         MKUU WA MKOA

        DAR ES SALAAM

AIBU: KAMANDA WA CHADEMA AJIANIKA JINSI ALIVYOKUBALI KUCHEZEWA NYETI ZAKE NA KUSAGWA NA JIKE MWENZAKE


Miezi michache baada  ya  kuvuja  kwa  video  inayomuonesha  mkurugenzi  wa  ulinzi  na  usalama  wa chama  cha  demokrasia  na  maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare  akidaiwa  kupanga  mauaji  ya  mwandishi  wa  habari,video  nyingine  ya  kamanda wa chama  hicho,Linda Bezuidenhout  imenaswa
  live....!!

Tofauti  na  video  ya  Lwakatare,hii  ya  Linda inaonesha  mambo  ya  aibu  sana  ambapo  mwanadada  huyo  amerekodiwa  akijieleza  NAMNA  ALIVYO  NUSURIKA  KUSAGWA  NA  MWANAMKE  MWENZAKE.....

Kwa  mujibu  wa  uchunguzi  wetu,Kamanda  huyu  wa  CHADEMA  alirekodiwa  kwa  ridhaa  yake  kwa  lengo  la  kumfikishia  ujumbe  huyo  mwanamke  kwa  uchafu  aliomfanyia....

Katika  video  hiyo, kamanda  huyo  wa  CHADEMA  alijieleza jinsi  alivyokuwa  anasagwa  na mwanamke  huyo....
"Mimi  nimefanya  wema, wema  wangu  umeniponza, wema  wangu  my assssss, wema  wangu  my  fangasi....msenge  we.

"Una wema  wewe?? Ungekuwa  na  wema  ungekuja  kushika  KU**********m  ya  dada  ako  wewe??....mshamba  mkubwa, huna adabu".   Alisema  dada  huyo

NAPE NNAUYE AYAKOROGA TENA



Nape Nnauye ameamua  kuvunja  ukimya  na  kutoa  utetezi  wake  kuhusu  kauli  yake chafu  iliyochapishwa  na  gazeti  la  Mtanzania  likimtuhumu  kuwatusi  wazee  waliopendekeza  uwepo  wa  serikali  tatu.....


Huu  ni  utetezi  wake:


"Nimestushwa sana na stori ya gazeti la Mtanzania inayodai kuninukuu kuwa nimesema wazee waliopendekeza serikali tatu wanasubiri kufa!

Kwakweli nimesikitishwa sana hata na jinsi maneno ndani yalivyopangiliwa kiasi kwamba inanipa tabu kuamini kama mhariri aliipitia hii stori ukiachilia mbali kama aliyetumwa kuja kuandika stori alikuwa ni "too junior".

Nawaheshimu sana wazee wangu hawa hata kama nikipishana nao kimawazo siwezi kufikia kutamka maneno makali kiasi hicho.

Nilichosema ni kuwa ukilinganisha vijana na wazee, vijana wana wajibu mkubwa wa kuamua kesho yao badala ya kudhani kuna mtu atawaamulia. Hivyo wana wajibu mkubwa kwani takwimu zinaonyesha asilimia 60% ya idadi ya watu nchini ni vijana! Sasa sijui kama kwa mwandishi na mhariri wake tafsiri ndio hiyo?!!!

Imenisikitisha  sana!

Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity"

ISHU NZIMA ILIVYOANZA:

Maji Yanavyowatesa Akinamama na Wanafunzi Kishapu

 

Mwanafunzi akifua sare za shule (kwanza kulia) wengine ni mabinti wakichota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
Mwanafunzi akichota maji katika visima vya muda Mto Tungu mara baada ya kutoka shule.
Na Joachim Mushi, Kishapu
WASWAHILI wanasema ‘maji ni uhai’ na maisha bila maji ni kadhia. Kimsingi mwanadamu anahitaji maji safi na salama katika kuendesha maisha yake ya kila siku. Na kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama eneo fulani huchangia kiwango fulani cha ugumu wa maisha kwenye familia.
Hali hii ndiyo inayowakumba wakazi wa baadhi ya vijiji vya Kata ya Kishapu, Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga. Tabu ya maji katika vijiji kama Lubaga, Isoso, Mwanuru pamoja na Kishapu yenyewe ni msamiati wa kawaida. Vijiji hivi hupata hauweni katika msimu wa masika pekee ambapo maji hutiririka hata kwenye mito ya msimu (masika).
Lakini mbali na familia kutaabika kusaka maji umbali mrefu kwa ajili ya matumizi ya kila siku, lipo kundi ambalo huathirika zaidi na kero za maji kwa kuwa kundi hilo ndilo linalotegemewa kutafuta maji katika familia kwa matumizi anua. Kundi hilo ni wanawake na watoto wakiwemo wanafunzi.

MBUNGE IDD AZAN ATUPIWA KOMBORA JIPYA



Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Iddi Azzan (pichani), aliyetajwa kwenye barua inayosadikiwa kuandikwa na wafungwa Wakitanzania waliopo Hong Kong “amejilisalimisha” kwenye ofisi za jeshi la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue mkondo wake.

Azzan amesema alienda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam.

"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike  na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azzan kwa njia ya simu



"Mimi sipo juu ya sheria ,  itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza:


 "Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao," alinukuliwa Mbunge huyo.

AHSANTE SANA KWA KWA KUJALI KWENU .... MWENYEZI MUNGU AWABARIKI SANA


MWALIMU NA MWANASIASA MKONGWE JOHN SHILATU AZIKWA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI

 Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu John Shilatu likiingizwa kwenye gari kutoka mochwari.

 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Shilatu likiwa mbele ya kadamnasa wakati wa Ibada

 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Shilatu likipelekwa eneo atakalozikiwa maeneo ya makaburi ya kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Makaburini Kinondoni
 Familia ya wafiwa wakiwa mbele ya jeneza
Jeneza lenye mwili wa marehemu John Shilatu likiingizwa kaburini ... Hakika ni huzuni kubwa sana isiyoelezeaka
Jeneza likiwa ndani ya kaburi
Mjane wa Marehemu Mama Shilatu akiwa udongo kaburini kwa Mume wake

 Mtoto wa Kwanza wa Marehemu Shilatu, Seba akiweka udongo kwenye kaburi la Baba yake
 Mtoto wa mwisho wa Marehemu, Digna naye pia akiweka udongo kaburini
 Mjukuu wa pekee wa Marehemu John Shilatu aitwaye Jayden akishiriki zoezi la kuweka udongo kwenye kaburi la Babu yake
DAIMA TUKAKUKUMBUKA JOHN SHILATU
MWENYEZI MUNGU AZIDI KUKUANGAZIA MWANGA WA MILELE KWANI MAISHA YAKO HAPA DUNIANI ULIMTUMIKIA KWA NGUVU ZAKO ZOTE

.... PICHA ZAIDI ZITAKUJIA BAADAE .....

HII HAPA RATIBA YA MAZISHI NA WASIFU ( RISALA ) YA MAREHEMU NDG JOHN SHILATU



RATIBA YA MAZISHI YA NDG. JOHN SHILATU 27 JULAI, 2013

A.
MUDA
TUKIO
MHUSIKA/WAHUSIKA
1.
02:00 – 03:00 ASUBUHI
KUPATA KIFUNGUA KINYWA
WAFIWA NA WAGENI
2.
03:00 – 05:00
KWAYA
VIKUNDI NA WAGENI
2.
05:00 – 06:00
CHAKULA
WOTE
3.
06:00 – 06:30 MCHANA
MWILI KUWASILI NYUMBANI
WAGENI/ FAMILIA YA MAREHEMU
4.
06:30 – 7:00 MCHANA
IBADA
(NYUMBANI)
WOTE
5.
07:00 – 07:15 MCHANA
WASIFU WA MAREHEMU
RODRICK
6.
07:15 – 07:20 MCHANA
NENO (A EUOLOGY)KUTOKA WATOTO WA MAREHEMU        NDUGU SHILATU
HELLEN
7.
07:20 – 07:30 MCHANA
NENO KUTOKA MCHUNGAJI
PASTOR JEREMIAH
8.
07:30 – 07:40 MCHANA
NENO KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI
MWENYEKITI
9.
07:40 – 08:40 MCHANA
KUTOA HESHIMA ZA MWISHO (NYUMBANI )
WOTE
10.
08:40 – 09:30 ALASIRI
KUELEKEA MAKABURINI
WOTE
11.
09:30 - 10:30 ALASIRI
MAZISHI
WOTE
12.
10 :30 JIONI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
WAHUSIKA

 
WASIFU WA MAREHEMU NDG. JOHN SHILATU
Aliyekuwa Baba, Babu, Mwalimu, Mwanansiasa na Kiongozi wetu Ndugu John Steven Shigemelo Shilatu alizaliwa Tarehe 24/06/1951 katika Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza akiwa ni Mtoto wa pili (2)  kati ya Watoto Watatu (3) ya familia ya Mzee Steven Shigemelo Shilatu na Mama Teje Mwanangeleja ambao wote ni kabila la Wasukuma wa mkoani Mwanza.
 
ELIMU:
Elimu ya Msingi: Mwaka 1959 alianza darasa la Kwanza katika shule ya msingi ya Bukandwe iliyopo katika kata ya Kisesa ambapo alisoma mpaka darasa la nne mwaka  1962 ambapo alihamia katika shule nyingine ya Msingi ya Bujora iliyopo Kata ya Kisesa ambapo alisoma darasa la tano mpaka darasa la nane kuanzia mwaka 1963 hadi mwaka 1966.
Elimu ya Sekondari: Mara baada ya kumaliza elimu ya msingi alifanikiwa kuwa Mwanafunzi wa pekee kati ya wote waliomaliza kufaulu na kupata fursa ya kujiunga na shule ya sekondari ya Bwiru iliyopo katika kata ya Kitangili Mwanza mjini ambapo alisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne kuanzia mwaka 1967 hadi 1970.
MAFUNZO:
Mara ya kumaliza elimu ya sekondari alifanikiwa kufaulu tena na kupata fursa ya kujiunga na chuo cha Ualimu cha Chang’ombe kilichokuwa kikiitwa Chang’ombe Teacher’s Training College kuanzia mwaka 1971 mpaka mwaka 1972.
Baada ya kumaliza digrii (Shahada) yake ya Ualimu alienda kupata mafunzo ya Kijeshi  ya muda wa miezi sita katika chuo cha kijeshi cha Mafinga - Iringa kilicho chini ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mnamo 1971 kwa mujibu ya utaratibu na sheria zilivyokuwa kabla ya kuajiliwa na Serikali.
KAZI:
Kutokana na ufaulu wake kuwa mkubwa sana akiwa chuoni, Mnamo tarehe 06.11.1972 kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo  alipata fursa ya kupata kazi ya ualimu ambapo aliteuliwa kuwa Mwalimu Mkuu wa kwanza kabisa Mwafrika katika shule ya Msingi ya Chang’ombe.
Kutokana na utendaji kazi wake bora wa ufauluishaji cha hali ya juu aliipatia shule ya Msingi ya Chang’ombe heshima ya kipekee kuwa shule bora ya msingi kitaifa kutokana na ufauluishaji bora na nidhamu bora aliyofanikiwa kuwajengea Walimu na Wanafunzi wa shule ya msingi ya Chang’ombe.
Alifanikiwa kuwa Mwalimu mkuu kwa takribani miaka 14 ya kuanzia mwaka 1972 hadi mwaka 1984
Mnamo tarehe 19/08/1998 alirudishwa tena kwenye kazi yake ya ualimu na kuwa Mwalimu wa shule ya msingi ya Chang’ombe na baadae shule ya Msingi ya Mtoni alipostaafu rasmi Ualimu mnamo Julai, 2011.
 
UONGOZI:
Katika enzi za uhai wa maisha yake, Marehemu John Shilatu alionyesha kipaji kikubwa cha uongozi tangu akiwa shule ya msingi na kpaji chake kilikuja kuonekana kitaifa mara baada ya kuwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Chang’ombe ambapo mnamo tarehe 11/01/1984 ilipelekea chama tawala Chama Cha Mapinduzi kumuazima kutoka katika Ualimu Mkuu na kwenda kufanya shughuli mbalimbali za kiuongozi ndani ya chama ambapo aliteuliwa kuwa Mkuu wa Idara Huduma za Umma CCM katika Wilaya ya Temeke kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987.
Mwaka tarehe 22/12/1987 alipanda daraja na kuwa Katibu wa Idara ya Huduma za Umma CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo alidumu na nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano mpaka mwaka 1992.
Mwaka 1988 mpaka mwaka 1994 alifanikiwa kuwa Diwani wa jiji la Dar es Salaam ambapo alifanikiwa pia kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Utamaduni Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam.
Mwaka 1989 mpaka mwaka 1991 aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Kariakoo Masoko
Mnamo tarehe 28/02/1995 aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Dk. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akishirikiana na Waziri Mkuu Cleopa David Msuya (wa kipindi hicho)alimteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga.
Mwaka 1997 alipadilishwa kituo cha Kazi na kupelekwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe iliyopo mkoani Shinyanga mpaka mwaka 1998.
Mnamo tarehe 26/08/1997 aliteuliwa kuwa Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Bukombe mpaka mwaka 2002.
Mnamo  tarehe 10/03/1998 Rais Benjamin Mkapa alisikiliza ushauri dhaifu wa aliyekuwa Waziri Mkuu Fredrick Sumaye (wa kipindi hicho) na kusitisha wadhifa wake wa Ukuu wa Wilaya.
Pia alishawahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM (W) Temeke kwa miaka 20 mfululizo.
Halikadhalika alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka 25 mfululizo.
Pia alikuwa Mjumbe wa Halmaushauri kuu ya Taifa (NEC) kwa muda wa miaka 10 mfululizo.
NDOA NA FAMILIA
Mnamo mwaka 1980 alifanikiwa kufunga ndoa ya pekee na Bernadina Joseph Makere, ndoa ambayo alidumu nayo mpaka umauti unamkuta
 Kwa takribani miaka 14 Ndugu John Shilatu alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali na umauti ulimkuta kutokana na shinikizo la damu ya kupanda ghafla usiku wa saa 8 tarehe 23/07/2013 na kupelekea mishipa ya damu kupasuka na kuvujisha damu ubongoni na hatimaye umauti kumkuta saa 9 alasiri ya tarehe 23/07/2013.
Marehemu Ndugu John Steven Shigemelo Shilatu ameacha mjane mmoja; Watoto watano ambao ni Benigna Shilatu (Akijiwe-Sebha), Emmanuel Shilatu (Chei au Buyegu), Geofrey Steven (Nondeji), Gerald John (Ntongeji) na Digna John (Wakubu-Shosha); na Mjukuu mmoja aitwaye Jayden.
Daima tutakukumbuka kwa malezi bora, upendo wa dhati uliokuwa nao kwa kila mtu, Ualimu uliotukuka, ucheshi na nasaha ulizotuachia.
MAVUMBINI TULITOKA NA MAVUMBINI TUTARUDI,
 
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
 
Amen!!




BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top