Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Profesa Kabudi awasha moto Katiba Mpya

Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi akifafanua jambo. Picha na Maktaba 
********
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi amejibu baadhi ya hoja za watu wanaopendekeza muundo wa serikali mbili na kusema Serikali ya Zanzibar ndiyo iliyoanza kutaka serikali tatu mwaka 1984.”
Aidha, amewashangaa wanaolibeza jina la Tanganyika kutumika serikalini kwa madai kuwa jina hilo siyo haramu kwa kuwa limo ndani ya Katiba ya sasa.

Alisema kuwa wakati huo madai ya serikali tatu yalitolewa na Zanzibar na kusimamiwa na Rais aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaji Aboud Jumbe.
“Hoja ilipelekwa pia kwenye Baraza la Wawakilishi, Brigedia Mstaafu Ramadhan Haji Fakhi (aliyekuwa Waziri Kiongozi), alikuwa akiongea kwa sauti nzito, kama ulikuwa ukimsikiliza, unasema muungano haupo,” alisema Profesa Kabudi na kueleza kuwa Fakhi alisema: “Zanzibar siyo koloni la Tanganyika.”
Alikuwa akichangia hotuba katika Kongamano la Kujadili Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika mjini Zanzibar jana. Alieleza kwamba mjadala wa sasa wa muungano siyo mkali kama uliokuwepo mwaka 1983 na 1984.
Hata hivyo, hotuba hiyo ya Profesa Kabudi iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) ilikatishwa kabla mzungumzaji kumaliza hotuba yake.
Katika maelezo yake, Profesa Kabudi ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kuwa Fakhi alikuwa haongei kama mtu baki, bali aliagizwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“Lugha ilikuwa ni kali,” alisema.
Akifungua kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal alisema kuwa masuala mengi yanayoleta mgogoro kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.
“Unawezekana kuwa muungano unatunyima fursa moja ua mbili, unatunyima uwezo wa kuamua katika masuala hayo, lakini wananchi hawayaoni hayo. Muungano ni wa wananchi, viongozi wana fursa zao, lakini wahakikishe wanawahudumia wananchi,” alisema.
Mjumbe huyo ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete na baadhi wanasiasa kutoka CCM, wakiwamo Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuikosoa Rasimu ya Katiba Mpya.
Kikwete pamoja na wajumbe hao kwa nyakati tofauti, walisema kuwa Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba haionyeshi uhalisia wa matakwa ya wananchi walio wengi kuhusu muundo wa muungano.
 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top