Frank
Mvungi-Maelezo
KAMATI ya Tanzania Kwanza nje ya Bunge la Katiba
imewataka Watanzania kutoyumbishwa na misimamo ya watu wachache wasioitakia
mema Tanzania.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Augustino Matefu wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar
es salaam.
Matefu
alisema kamati hiyo imeona ni vyema ikawahamasisha Watanzania kuungana na kuwa
na mshikamano katika kipindi hiki cha mchakato wa Katiba mpya ili Taifa
liwezekuwa na ustawi.
“Sisi kama
vijana wazalendo tumeweka Utaifa kwanza vyama baadae ili kuwahamasisha vijana kote nchini
kushikamana na kulinda Tunu za Taifa letu na kupinga kwa dhati wale wote wanaotaka kwenda kinyume na misingi
madhubuti iliyowekwa na waasisi wa Taifa Letu”, alisema Matefu.
Alieleza
kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa
wanaweka maslahi ya Taifa kwanza na vyama vyao baadae ili Malengo ya mchakato
wa Katiba mpya yaweze kufikiwa.
Naye Mjumbe
wa Kamati hiyo, Renatus Muabi alisema kuwa ni vyema Watanzania wote wakaungana
katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba mpya na kufanya kila jambo kwa kuzingatia umuhimu
wa Katiba mpya na kuacha itikadi za vyama vyao ili kutoa kipaumbele kwa mambo
yenye maslahi kwa Taifa.
Kamati ya
Tanzania Kwanza nje ya Bunge imeandaa
maandano ya amani na Mikutano ya hadhara kikanda katika kanda ya Kaskazini,Nyanda za Juu Kusini,Kanda ya
Magharibi,Kanda ya Kati.
Maandamano
na mikutano hiyo itafanyika pia katika Kanda ya Kusini,Kanda ya Mashariki,Kanda
ya Mwanza,Zanzibar na Unguja huku lengo likiwa ni Kuhamasisha umoja na
mshikamano miongoni mwa Watanzania katika kipindi hichi cha mchakato wa Katiba
mpya.
Kamati ya
Tanzania Kwanza nje ya Bunge la Katiba imeundwa na wajumbe toka vyama 7 vya
siasa hapa nchini wakiwa na lengo moja la kuhamasisha
Post a Comment