
- MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IYALA AMEKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA NA WATU WASIOFAHAMIKA.
- MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI WILAYANI MBARALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWANANYELA KALIMANZILA (43) MKAZI WA
KIJIJI CHA IYALA ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI
ZA MWILI WAKE NA MTU ASIYEFAHAMIKA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 04.05.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA IYALA, KATA YA CHIMALA, TARAFA YA ILONGO WILAYA YA
MBARALI MKOA WA MBEYA. INAELEZWA KUWA MAREHEMU ALITOWEKA NYUMBANI KWAKE
TANGU TAREHE 03.05.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI AKIWA NA MTOTO WAKE
WAKIELEKEA SHAMBANI UMBALI WA KILOMITA 170, WAKIWA SHAMBANI NDIPO
ALITOKEA MTU ALIKUWA AMEJIFUNGA MATAMBALA USONI NA KISHA KUANZA KUMKATA
MAPANGA. CHANZO CHA TUKIO HILI NI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA. MUME WA
MAREHEMU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KALIMANZILA MAGOFI (70) ANASHIKILIWA
NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANA ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILI KWANI
INADAIWA KUWA ALIKUWA AKIMTUHUMU MKEWE KUWA ANAMROGA. JUHUDI ZA
KUWATAFUTA WATU WENGINE WALIOHUSIKA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA
NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA
KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BROWN MOGA (80) MKAZI WA KIGOE
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA NAMBA
ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO 04.05.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO KATIKA
KIJIJI CHA KIGOE, KATA YA MAHONGOLE, TARAFA YA ILONGO WILAYA YA MBARALI
BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA
ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA
MIGUU KUTEMBEA PEMBEA MWA BARABARA NA KUVUKA SEHEMU ZENYE VIVUKO ILI
KUEPUKA AJALI .AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA MSAKO:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MADIBA BUHEMBO @ CHEREHANI (42) MKAZI
WA KIMBEREKETE-MAPUGORO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA ROBO HEKTA.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA KIMBEREKETE, KIJIJI CHA MAPUGORO, KATA YA CHOKAA,
TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. BHANGI HIYO INA
UREFU WA FUTI SABA [07]. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KULIMA ZAO HARAMU LA BHANGI KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJISHUGHULISHE NA KILIMO CHA
MAZAO MENGINE YA CHAKULA/BIASHARA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment