Watu watatu
wa familia moja, wakazi wa Kijiji cha Kwasunga wilayani Handeni wamekufa
baada ya kula futari ya mihogo inayosadikiwa kuwa na sumu.Akizungumza
na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga,
Constantine Massawe alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku
eneo la Kwasunga Handeni na maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Handeni.Kamanda Massawe aliwataja waliokufa kuwa ni Juma Jumbe
(6), Abdi Jumbe (10) na Ramadhani Jumbe (15). Pia alisema kuwa wazazi
wa watoto waliwahishwa hospitali ambako walipatiwa matibabu na
wanaendelea vizuri.
Kamanda
Massawe alisema kwa mujibu wa wazazi wa watoto hao, walikula futari hiyo
na baada ya kumaliza, walianza kujihisi vibaya sambamba na kuishiwa
nguvu na alianza kuanguka mmoja baada ya mwingine.“Chanzo cha kifo ni
futari ya mihogo ambayo kwa mujibu wa vipimo ilikuwa na sumu. Wazazi wao
wako hai ila nao walikuwa katika hali mbaya, lakini baada ya kupatiwa
matibabu wanaendelea vizuri,” alisema kamanda huyo.Kamanda huyo
aliwataka wote walio katika mfungo kuichunguza mihogo wanayoinunua kwa
ajili ya matumizi ya futari kwani baadhi haifai kuliwa na binadamu.Mhogo
unajulikana vyema. Kama mtu ukiumenya na kuona una rangi za ajabu ajabu
ndani, basi achana nao usiupike mingine haifai kuliwa na binadamu,”
alisema Massawe. Alitoa wito kwa watu kuwa makini. (MWANANCHI)
Post a Comment