MBUNGE WA KAHAMA MH JAMES LEMBELI
‘Mimi nilivyozomewa mwaka 2010 mbele ya Rais Jakaya Kikwete nilijifunza mengi na leo hii siwezi kuzomewa tena.” James Limbeli
Mbunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli amewataka wananchi kuwazomea madiwani wazembe wasioleta maendeleo yaliyo ndani ya uwezo wao.
Kauli hiyo aliitoa juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mayila, Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Lembeli alisema ni haki ya wananchi kuwazomea madiwani wa aina hiyo.
Kauli hiyo ilikuja baada ya wananchi kulalamikia
ubovu wa barabara katika mtaa huo, ambao walidai kwa miaka 17 iliyopita,
eneo hilo halijawahi kufanyiwa matengenezo ya miundombinu yake.
Alisema pamoja na mambo makubwa aliyofanya diwani
wa eneo hilo, Amosi Sipemba, siyo mwisho wa kuleta maendeleo mengine
ambayo yapo chini ya halmashauri na kwamba diwani anahudhuria vikao
vyote vya uamuzi.
“Suala la barabara ni la diwani wenu, mimi kazi
yangu ni kusukuma tu kwa kuwa jimbo langu lina kata 34, hivyo ni vigumu
kutambua matatizo ya wananchi bila kupitia kwa diwani. Mwambieni diwani
wenu na atanifikishia,” alisema Lembeli na kuongeza:
“Huyu mkimwambia atanifikishia nami, nitakwenda
kusukuma huko kwenye halmashauri, mwambieni ikibidi mzomeeni ili
akamweleze mke wake alivyozomewa.
Mimi nilivyozomewa mwaka 2010 mbele ya Rais nilijifunza mengi na leo hii siwezi kuzomewa tena.”
Mimi nilivyozomewa mwaka 2010 mbele ya Rais nilijifunza mengi na leo hii siwezi kuzomewa tena.”
Hata hivyo, kabla ya hapo Diwani wa Kata ya
Nyihogo, Sipemba alisema tangu aingie madarakani mwaka 2010 hakukuwa na
barabara yoyote iliyochongwa katika eneo hilo, lakini hadi sasa asilimia
kubwa zimefanyiwa matengenezo.
Akizungumzia kuhusu kuzomewa na wananchi, Sipemba
alisema yeye siyo mhandisi wa kutengeneza barabara na kwamba hata yeye
pia anaomba kutoka halmashauri ya mji.
SOURCE:MWANANCHI
SOURCE:MWANANCHI
Post a Comment