Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

"MAFANIKIO YETU YANATOKANA NA WANAUME AU WAPENZI WETU" ASEMA AUNT EZEKIEL


STAA wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel, amesema mafanikio ya wasanii wengi wa kike hayatokani na mauzo ya kazi hiyo bali sapoti ya waume au wapenzi wao kwa kuwa soko la filamu limeharibika.
 
“Filamu kwa Tanzania hakuna soko, walau wanaume, si wanawake, huwezi kunilinganisha mimi na Ray… Mimi kama si kuwa mwanamke, sidhani kama leo hii bado ningekuwepo katika filamu, kwa sababu kwa kiasi kikubwa nategemea sapoti ya wadau wangu, si mauzo ya filamu,” alisema.
 
Aunt alisema tatizo jingine katika soko la filamu nchini, ni wasanii kutopendana hali ambayo inashusha tasnia kila kukicha. Kwamba wangekuwa na mshikamano, wangeweza kufanya kitu cha kuwasaidia katika kuiboresha.
 
“Umoja ndiyo kila kitu hata kama tutakuwa hatuna hela, lakini tukikaa watu wengi kujadili kitu fulani, tutajua tufanye nini, hata kimawazo tu tutaendelea,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top