Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa
zitakazofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam.
Askari
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi
katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu
ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Askari
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi
katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu
ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar
es salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya
Mashujaa itakayofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Saidi Meck Sadiki amesema kuwa maadalizi ya sherehe hizo
yamekamilika na kuongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu kihistoria
yanalenga kuwaenzi wote waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa
ardhi ya Tanzania, kuilinda na kudumisha amani na utulivu uliopo.
Amesema
maadhimisho hayo yatapambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Gwaride la
Kumbukumbu litakaloonyeshwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Jeshi la Magereza na Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT). Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na
uwekaji na silaha za asili, maua kwenye mnara wa kumbukumbu pamoja na
viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kutoa dua na sala kuliombea
taifa.
Bw.
Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja
zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana, pia wananchi
watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio
yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa
zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja huo. Aidha, katika
hatua nyingine ameeleza kuwa wakati wa maadhimisho hayo barabara ya
Lumumba, Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda kwa lengo la kuhakikisha
usalama kwa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho
hayo.
Post a Comment