Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA NHC


1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe akisoma taarifa ya shirika hilo kukanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku na mitandao ya kijamii kuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu Kyando ameundiwa zengwe na baadhi ya wabunge ili aondolewe katika shirika hilo, wanaofuaia katika picha ni Muungano Saguya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii, Bw. Martin Mdoe Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Benedict Kilimba Mkurugenzi wa Uendeshaji Miliki
2
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe akisoma taarifa ya NHC kulia ni Mpnda Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi .
....................................................................................
Utangulizi: Jumatatu na Jumanne ya wiki hii, kumekuwa na taarifa zilizochapishwa kwenye moja ya gazeti la kila siku zikieleza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Kyando Mchechu ameundiwa zengwe na Bodi ya Wakurugenzi ya NHC kwa nia ya kuhakikisha kuwa harejeshwi tena katika wadhifa huo, hasa baada ya Bw. Mchechu kumaliza muda wake wa kuliongoza Shirika hili. Aidha, gazeti hilo liliwaaminisha umma wa watanzania kuwa mizengwe hiyo inaungwa mkono na vigogo wa Serikali wakiwemo Wabunge ambao kuwepo kwa Bw. Mchechu katika Shirika kumewanyima ulaji ikiwemo kupangishwa nyumba za Shirika. Gazeti lililienda mbali zaidi likidai kuwa Bw. Mchechu amewekewa masharti magumu na Bodi hiyo ya kumtaka apunguze idadi ya Wakurugenzi wa Menejimenti ya sasa ya Shirika.

Kwa kuwa habari hizo zimeleta mtafaruku katika Shirika na zimesababisha umma kuwa na mijadala mbalimbali juu ya jambo hili, tungependa kuwataarifu umma kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote, na Shirika la Nyumba la Taifa linapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:-
1. Kwanza, ifahamike kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC ina miezi miwili tu tangu iteuliwe na Mamlaka husika na haijawahi kukaa katika kikao chochote kujadili suala la kumuondoa Mkurugenzi Mkuu na kupunguza Menejimenti ya Shirika iliyopo sasa.

2. Tunapenda kuwafahamisha kuwa Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya Shirika bado wana mikataba halali ambayo haijamalizika muda wake, hivyo hoja ya kuwa Bwana Mchechu na Menejimenti yake wanaundiwa zengwe baada ya kumaliza muda wao haina ukweli wowote.

3. Kwamba kutokuwepo kwa Mkurugenzi Mkuu kwenye ufunguzi wa miradi hakukutokana na kuwepo mizengwe kama ilivyoripotiwa na Gazeti hili. Bw. Mchechu alikuwa katika likizo yake ya mwaka iliyooanza tarehe 30 Juni na kumalizika Julai 18, 2014. Likizo hii ni stahili halali ya Bw. Mchechu kama walivyo watumishi wengine wa umma, na hakuichukua likizo hii kutokana na kuwepo mizengwe ya kumuondoa kama ilivyoripotiwa na Gazeti hili. Kuanzia tarehe 21 Julai, 2014 Bw. Mchechu yupo kikazi nje ya nchi na anatarajiwa kuwa ofisini kwake tarehe 28 Julai, 2014.

4. Mwisho, tunapenda kuwatanabaisha wanahabari kuwa kama ilivyo kawaida yetu, NHC imekuwa na itaendelea kuwa mstari wa mbele kutoa habari makini kwa vyombo/chombo chochote cha habari bila kuficha jambo lolote. Hivyo, tunawaomba muendelee kuitumia vyema fursa hii kupata habari zenye ukweli na zilizo sahihi kwa jambo lolote mnalohitaji kuufahamisha umma wa watanzania. Kwa kufanya hivyo, tutaendelea kuwa washirika wakubwa wa vyombo vya habari, tukizingatia kuwa vyombo vya habari vina dhima na dhamana kubwa katika kuleta tija kubwa kwa Shirika na Taifa letu. Aidha, tunawafahamisha wateja wetu kuwa hakuna mtafaruku wowote uliyopo ndani ya Shirika la Nyumba la Taifa na kwamba tunaendelea kuwapa huduma zetu zilizo bora katika sekta ya nyumba tuliyoaminiwa na Taifa kuisimamia.

IMETOLEWA NA:
BW. DAVID SHAMBWE,
KAIMU MKURUGENZI MKUU
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top