Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI WA MAZINGIRA DKT. BINILITH MAHENGE ATOA MIEZI MINNE KWA KIWANDA CHA M.M.I STEEL MILLS KUHIFADH MAZINGIRA

6 - Copy - Copy


1 - Copy - Copy   
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge (katikati) akiambatana na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda cha M.M Integrated Steel Mills Ltd, Lawrence Manyama (kulia) wakati walipowasili kwenye kiwanda hicho kwa ukaguzi.Kushoto ni Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC)Manchare heche.
2.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge (mwenye koti la bluu) akijadili jambo na maafisa wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) juu ya mchanganyiko wa mabaki ya madini yanayotumika kwenye kiwanda cha M.M Integrated Steel Mills Ltd.

6 - Copy - Copy
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge( kulia) akitoa msiamamo wa Serikali kuhusu kiwanda hicho baada ya kukikagua.Katikati ni Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda cha M.M Integrated Steel Mills Ltd, Lawrence Manyama na Mkuu wa Biashara wa kiwanda hicho Shashikant Modi .
5 - Copy - Copy
Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda cha M.M Integrated Steel Mills Ltd, Lawrence Manyama (katikati), akitoa maelezo kuhusu kiwanda hicho.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge na kushoto ni Mkuu wa Biashara wa kiwanda hicho Shashikant Modi .
7 - Copy - Copy
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge, akitoa maelekezo kwa wamiliki wa kiwanda cha BIDCO Oil & Soap Ltd( hawapo pichani) juu ya kusitisha kutumia magogo kama chanzo cha nishati.Aliyevaa overall ya njano ni Msimamizi Mkuu wa kiwanda hicho David Kiawa akimsikiliza.
8 - Copy - Copy
Meneja Mkazi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Cocacola Kwanza, Luois Coetzee (mwenye kofia nyekundu) akimweleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge (mwenye koti la bluu) kuhusu tangisamaki kama kiashiria cha ubora wa majitaka yanaotibiwa na kiwanda hicho.
9 - Copy - Copy
Meneja Mkazi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Cocacola Kwanza, Luois Coetzee (mwenye kofia nyekundu) akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge, jinsi soda zinavyotengenezwa na kukaguliwa kwenye kiwanda hicho.Kulia ni mfanyakazi anayekagua soda zilizotengenezwa kabla ya kupakiwa.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO.
4 - Copy - Copy
Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda cha M.M Integrated Steel Mills Ltd, Lawrence Manyama (anayeonesha chini) akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge( kulia kwake) sehemu yenye mchanganyiko wa mabaki ya madini yanayotumika kiwandani hapo.
………………………………………………………..
Hussein Makame-MAELEZO
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahende ametoa miezi minne kwa kiwanda cha M.M Integrated Steel Mills Ltd kiwe kimefunga mitambo ya kutibu majitaka yanayozalishwa na kiwanda chao .
Waziri Dkt. Mahenge alitangaza hatua hiyo wakati akiwa kwenye ukaguzi kwenye kiwada hicho kilichopo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mfululizo wa ukaguzi anaoendelea kuufanya kwenye viwanda mbalimbali jijini humo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) iliyo chini ya ofisi hiyo, kupokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa Chuo cha Kodi kilicho jirani na kiwanda hicho kuwa wanaathirika na majitaka ya kiwanda hicho.
Mbali na kupewa sharti la kufunga mitambo hiyo, Waziri Dkt. Mahenge aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuwasilisha Mpango wa Kuhifadhi Mazingira wa kiwanda hicho baada ya miezi mitatu ambao kuwepo kwake kunatiliwa shaka.
Hatua hiyo ilitokana na kiwanda hicho kushindwa kumridhisha waziri juu ya wapi wanaupeleka mchanganyiko wa mabaki ya madini mbalimbali yanayotumiwa na kiwanda hicho baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa hutumika kinyume na taratibu.
Mbali na hayo, Waziri Dkt. Mahenge alitoa miezi mitatu wawasilishe ripoti ya ukaguzi wa mazingira kinyume cha hapo watatozwa faini na NEMC kwa mujibu wa sheria kwani hawaruhusiwi kuendesha kiwanda katika hali hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa kiwanda hicho Mkurugenzi wa Miradi ya kiwanda hicho, Lawrence Manyama alisema watatekeleza maagizo hayo ingawa alidai kwa sasa wameacha kugawa mchanganyiko wa madini kwenye viwanda.
Katika kiwanda cha BIDCO Oil & Soap Ltd, Waziri huyo alitoa muda wa miezi 6 kwa kiwanda hicho kuacha kutumia magogo ya miti kama vyanzo vya nishati kwani matumizi hayo yanachangia kuharibu mazingira.
Alisema gharama za kukabilaiana na mabadiliko ya tabianchi yanayochangiwa na matumizi ya chanzo hicho ni kubwa sana kwa Serikali lakini pia kwa karne ya sasa kiwanda hicho kinatakiwa kuacha kutumia chanzo hicho.
Hata hivyo, mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho Elias Nchwari aliponea chupuchupu kuwekwa ndani ya Mwanasheria wa NEMC Manchare Heche,baada ya kumjibu vibaya Waziri Dkt. Mahenge wakati aliwasili kwenye kiwanda hicho.
Katika hatua nyingine Waziri Dkt. Mahenge alikipongeza kiwanda cha Cocacola Kwanza kwa kupiga hatua kubwa ya mabadiliko ya matumizi ya nishati na katika kuhifadhi mazingira kwa kutumia mitambo ya kisasa kutibu majitaka.
Hata hivyo, aliutaka uongozi wa kiwanda hicho uwe mabalozi kwa viwanda vingine ambavyo havizingatii kuhifadhi mazingira katika uzalishaji wao, hivyo kuwa chanzo kikubwa cha kuchafua mazingira.
Naye Meneja Mkazi wa Uzalishaji wa kiwanda hicho Luois Coetzee alisema pamoja na gharamu kubwa waliyotumia katika nishati na mitambo ya kutakatisha majitaka, lengo lao kubwa na kuhakikisha wanafanya mambo kwa usahihi wake.
Mtaalamu wa Mitambo ya Kutakatisha Majitaka Emiliana Kweka alisema wanalazimika kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa maji yanayotoka kwenye kiwanda hicho yanakuwa salama kwa mazingira na viumbehai.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top