Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Fahamu alichoamua Kingwendu baada ya mkewe KUBAKWA akiwa amelewa


Muigizaji wa filamu za Kiswahili, mchekeshaji Kingwendu yuko katika wakati mgumu baada ya mkewe kubakwa na jirani yake wakati akiwa amelewa pombe.
Baada ya jitihada nyingi za kumtafuta Kingwendu, hatimaye mwandishi alifanikiwa kumpata na kukiri kuwa alizipata habari hizo wakati ambapo yuko safarini na majirani walimueleza kilichotokea kuwa mkewe na jirani huyo aliyembaka mida ya saa tano usiku wote walikuwa wamelewa.
”Kama ulivyosikia hiyo habari, mimi nilikuwa sipo ndo nimerudi juzi, nataka nianze kufuatilia sheria sema sasa hivi nimefiwa na dada yangu tunapeleka msiba kijijini na baada ya hapo ninapumzika halafu ninasafiri Nairobi, nikirudi Nairobi tarehe tano kuanzia tarehe sita ndo naanza kufuatilia.” Amesema Kingwendu.
Mchekeshajihuyo ameumizwa na kitendo hicho na ameamua kufuata taratibu za kisheria ili haki itendeke.
“Kutokana na kitendo alichokifanya na mimi nimejisikia vibaya, inanibidi nimtafute huyu bwana nimpate ili nimpeleke mahakamani, mke wangu bado niko naye, sema huyu jamaa aliyefanya unyamaa huu yupo jirani. Mke wangu alikuwa amelewa na jamaa naye alikuwa amelewa. Mke wangu sijui alikuwa anatoka wapi saa tano usiku ndo akakutana na huyo jamaa, majirani ndio walivyoniambia hivyo, walinipigia simu wakati nipo Shinyanga huko.” Amesema Kingwendu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top