Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TANESCO YAMNASA KISHOKA MAARUFU MKOANI PWANI

 


SHIRIKA la Ugavi wa Umeme (Tanesco) Mkoa Pwani, limefanikiwa kumkamata Jeams Mkelembwa ambaye anadaiwa kuwatapeli wananchi kwa kujifanya mtumishi wa shirika hilo.
Akizungumza kuhusu sakata hilo jana, Ofisa Usalama wa Tanesco Pwani, Henry Byarugaba, alisema kwamba tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa  huyo lilitokea juzi wilayani Kisarawe wakati alipokuwa akitaka kumtapeli mteja mmoja  wa umeme.
Byarugaba alisema mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia njia mbalimbali ikiwemo kutumia majina ya viongozi, pamoja na kudai yeye ndiye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani, kitu ambacho si cha kweli.
“Ndugu mwandishi, katika siku za hivi karibuni tulikuwa na zoezi maalumu la kukagua miundombinu yetu ya umeme katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani, lakini tulipata fununu kuna baadhi ya watu wanajifanya wao ni wafanyakazi wa shirika letu na kuwatapeli wateja wetu, hali ambayo inasababisha lawama nyingi kutolewa kwetu…
“Huyu jamaa tuliyemkamata ni hatari sana, kwani ameshafanya matukio mengi ya utapeli kwa wananchi, maana anatumia vyeo vya watu mbalimbali ikiwemo kujifanya yeye ni ofisa wa Tanesco, mara mtumishi kutoka wizara fulani mara Takukuru, yaani ni balaa tupu, kumbe ni kishoka maarufu sana na mimi nitahakikisha anachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho,” alisema Byarugaba.
Alisema mtuhumiwa huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi Kisarawe na kuwaomba wateja wote ambao wametapeliwa na mtu huyo waende kwa ajili ya kumtambua.
Byarugaba aliongeza kuwa tapeli huyo alishafanya matukio ya kuwaibia watu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Majohe, Pugu, Chanika na mengineyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top