Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAARIFA: MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII 2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA

MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII 2014

Wizara ya Maliasili na Utalii  kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Arusha  pamoja na Wadau wa Sekta ya Utalii nchini wanayofuraha ya kuwakaribisha   Wananchi wote  na Wadau mbalimbali  katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani   kwa mwaka 2014  ambayo  Kitaifa yatafanyika  Mkoani Arusha kwenye viwanja vya  Nane Nane (TASO) kuanzia tarehe 20 hadi 28 Septemba, 2014.
Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ambapo kila nchi  mwanachama wa Shirika  la Utalii Duniani (UNWTO) husherekea siku hii, kwa lengo la kuweka uelewa kwa Jamii kuhusu umuhimu wa utalii na thamani yake, kijamii, kisiasa, kitamaduni na kiuchumi.
Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni “Utalii na Maendeleo ya Jamii’’ (Tourism and Community Development) kwa kuzingatia Kauli Mbiu hii,  tunawajulisha wadau wote katika nyanja mbalimbali za Utalii, Maliasili na Uhifadhi, vikundi vya jamii na wajasiriamali, viongozi na wataalamu kwa pamoja kushiriki kikamilifu katika  Maadhimisho ya  Siku ya Utalii Duniani kwa nia ya kujifunza na kutambua fursa za kiuchumi zilizopo katika Sekta ya Utalii na kutumia fursa hizo kujikomboa katika umaskini.
Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kuwasilisha na kuonesha na kwa vitendo juu ya tafsiri ya Kauli Mbiu kwa kufanya kongamano la  ushirikishwaji wa jamii kwenye sekta ya Utalii kwa ajili ya kujiletea maendeleo, mashindano ya Uchoraji wa picha kuhusiana na kauli mbiu, michezo na burudani mbalimbali.
Vilevile kutakuwa na maonesho ya utalii, malikale, misitu na masuala ya uhifadhi kwa ujumla na bila kusahau ziara ya kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na  Hifadhi ya Taifa ya  Arusha  kwa nia ya kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye shughuli za utalii wa ndani.
Wito unatolewa kwa kuwaalika wadau wote wa utalii na jamii husika kuja kwa pamoja na kuadhimisha siku hii kama ishara ya jitihada za pamoja za kufanya utalii nguzo ya kweli ya maendeleo ya Jamii nchini.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top