Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHADEMA WATANGAZA KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA KATIBA INAYOPENDEKEZWA

 

Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimesema kinakamilisha ushahidi ili kwenda mahakamani kupinga katiba inayopendekezwa kupelekwa katika hatua ya kupigiwa kura ya maoni kwa madai kuwa katiba hiyo imekosa uhalali kutokana na kukosa theluthi mbili kutoka upande wa Zanzibar.
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara Profesa Abdalah Safari ametoa tamkoa hilo wakati akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake kwenye uwanja wa Mlandege ambapo amebainisha kuwa zoezi la kupitisha rasimu ya katiba inayopendekezwa ndani ya Bunge maalumu la katiba liligubikwa na mbinu chafu za uchakachuaji wa kura hasa za wajumbe wa Zanzibar.
 
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Dokta Wilbrod Slaa amesema chama cha mapinduzi kimeanza kuhujumu mchakato wa uandikishaji wa wananchi kwenye Daftarai la Makazi kwa kuendesha zoezi hilo kwa siri huku kikitumia mabalozi wa nyumba kumi wa chama hicho kinyume na utaratibu wa kawaida ambapo kazi hiyo inapaswa kufanywa na watendaji wa vijiji kata na mitaa.
 
Aidha katibu mkuu huyo wa Chadema amewataka wananchi kutodanganyika na vipengele vya haki za makundi mbalimbali zilizowekwa kwenye katiba hiyo pendekezwa akieleza kuwa zimewekwa kama chambo kwani haki hizo zimeondolewa na kifungu cha 21 kinachoeleza kuwa haki hizo hazitadaiwa mahakamani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top