Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MFANYABIASHARA AJIUA KWA KUNYWA SUMU NYUMBANI KWA BABA MKWE


MFANYABIASHARA wa mjini Tarime mkoani Mara, Wilson Weso maarufu Kishimba (34) amekufa kwa kile alichodaiwa amekunywa sumu nyumbani kwa baba mkwe wake.
 
Inadaiwa alifanya hivyo nyumbani kwa baba mkwe, Chacha Sasita ambaye ni mkazi wa kijiji cha Rebu kata ya Turwa, kutokana na mgogoro na mke aliyemtoroka na kwenda jijini Mwanza na kumwachia watoto wawili.
 
Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Lazaro Mambosasa alisema kifo hicho kilitokea juzi.
 
“Alifariki dunia kwa kunywa kitu kinachodhaniwa ni sumu,” alisema kamanda.
 
Kwa mujibu wa kamanda, baada ya mke wa mfanyabiashara huyo kuondoka, alichukua watoto alioachiwa na kuwapeleka kwa baba mkwe kabla ya kunywa sumu.
 
"Mwili wa marehemu uligunduliwa muda mchache na wakazi wa kijiji hicho cha Rebu ambapo askari wetu walifika na kuuchukua mwili huo na kuupeleka chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya kwa uchunguzi zaidi,” alisema Kamanda huyo na kuongeza kwamba polisi inaendelea na uchunguzi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top