Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Taarifa Rasmi ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Waziri Kuhusu Taarifa Za Huduma Dhoofu Hospitalini na Deni la Serikali Kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD)

 

 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii  Dkt. Seif S. rashidi (Mb)
 --
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Kuna taarifa katika vyombo vya habari iliyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA, kwamba serikali haijalipa kiasi cha shilingi bilioni 90 kwa bohari kuu ya dawa na kusababishia ukosefu dawa katika baadhi ya hospitali.

Ni kweli bohari kuu ya dawa imepungukiwa fedha za kununulia dawa, lakini sio kwa kiasi cha kushindwa kutoa huduma kabisa kama inavyoelezwa. Kiasi cha pesa kinachotajwa si kigeni na serikali imekua ikitoa kiasi cha fedha kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa bohari ya dawa iweze kufanya kazi ya kununua na kusambaza dawa.

Katika kukabiliana na hali hii hospitali zote kupitia waganga wakuu wa mikoa na wilaya zimeagizwa kupeleka asilimia 50 ya mapato yanayotokana na uchangiaji kwenda bohari kuu ya dawa.
Kuhusu ukosefu wa matibabu katika Taasisi ya Saratani ocean road, ni kweli kwa sasa baadhi ya mashine hazifanyi kazi na zinazofanya kazi ni chache hivyo kuzidiwa wakati fulani. Hata hivyo Wizara imekwisha agiza vifaa hivyo ambavyo ni ghali sana toka Canada na vinategemewa kufika wakati wowote kuanzia sasa na pia ikumbukwe kuwa matibabu yanatotolewa bila malipo na gharama zote ni za serikali.

Wizara kwa sasa imeagizwa katika mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) ambapo wataalam wanamalizia kazi za utekelezaji wa mpango huo. Ambapo pia umezingatia namna ya kukabiliana na jinsi ya kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati katika vituo vya matibabu na kuiboresha zaidi bohari ya dawa. Baada ya kuanza utekelezaji huo suala la ukosefu wa dawa na vifaa tiba utapungua kwa kiasi kikubwa sana.

Pamoja na wizara kupeleka bohari tyadawa pesa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hospitali zihakikishe zinapeleka asilimia 50 ya mapato kama zilivyoagizwa na kutokufanya hivyo kiongozi husika atawajibishwa.

Mwisho wizara inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba dawa na vifaa tiba muhimu vinapelekwa katika vituo vyote, pia inaendelea kufanya kazi na taasisi zote zisizo za kiserikali kwa karibu kwa faida ya wananchi wote.
Imetolewa na :-

Dkt. Seif S. rashidi (Mb)
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII
27/10/2014
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top