Serikali
imepokea mabehewa 50 ya mizigo na mabehewa 22 ya kisasa ya abiria ikiwa
ni sehemu ya mabehewa 274 yanayotawarajiwa kuwasili nchni ili kuboresha
huduma za usafiri wa mizigo na abiria hapa Nchni.
Akizungumza
na waandishi wa habari, waziri wa uchukuzi Daktari Harrison Mwakyembe
amesema kuingia kwa mabehewa hayo ni ishara ya jitihada za serikali
katika kuimarisha huduma ya usafiri wa reli ambapo amesema amesisitiza
serikali imetumia zaidi ya bilioni 200 katika kuboresha sekta ya reli
nchni.
Kwa
upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la reli nchni Bwana Kipalo
Kisamvu amesema mabehewa hayo ya abiria ni kwa ajili ya safari katika
mikoa ya mwanza na kigoma, na kusisitiza shirika hilo la Reli kwa
kushirikiana na wakala wa usafiri wa majini na nchi kavu wako katika
mchakato wa kuanzisha usafiri wa haraka wa abiria ambao utasimama katika
vituo vikubwa pekee. (Picha na Ernest Nyambo)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na
Waziri wa Uchukuzi, Dr. Harrison Mwakyembe wakikagyua moja ya mabehewa
mapya ya TRL yaliyonunuliwa kwa fedha ya serikali wakati alipokwenda
kwenye Bandari ya Dar es salaam Desemba 8, 2014 kupokea mabehewa
hayo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dr. Harrison
Mwakyembe (kulia kwake) na Naibu Waziri wake, Dr. Charles Tizeba
(kulia) kukagua baadhi ya mabehewa mapya ya Shirika la Reli nchini
(TRL) yaliyonunuliwa na kwa fedha za serikali wakati alipokwenda kwenye
bandari ya Dar es salaam Desemba 8,2014.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Post a Comment