Zikiwa zimebaki siku tano kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa nchini, Katibu wa Kata ya Kisutu, Dar es Salaam wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sauda Addy na Mjumbe wa Kamati ya Udhamini ya Chama Cha Demekrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassan, wamepigana.
Sababu
za kupigana kwao zinatokana na Hassan kuchana bango la mgombea wa CCM
wa nafasi ya Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kisutu ambalo lilibandikwa
katika ofisi yake ambayo ni jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti jana na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam,
katika ofisi ya Makao Makuu ya Polisi mkoa, walisema tukio hilo
lilitokea Desemba 6 wakati Sauda alipofika katika ofisi ya Hassan
kumshutumu kutokana na kitendo cha kuchana bango hilo.
Hassan,
alisema siku ya tukio Sauda alifika ofisini hapo na kuanza kumshambulia
kwa maneno na kipigo, hivyo watu kuingilia kati ili kuamulia vurugu
hizo hali iliyosababisha akapoteza vitu vyake ikiwamo, miwani, nyaraka
za ofisi na kuharibu samani za ofisi.
Sauda
alisema siku ya tukio alimfuata Hassan ili kuhoji sababu za kuchana
bango walilokuwa wamebandika, lakini cha kushangaza alimkunja nguo yake
ya juu na kukata kifungo hali iliyomlazimu kwenda kituo cha polisi
kuripoti.
Wote
waliripoti katika kituo kidogo cha Polisi Kisutu na kutakiwa kuripoti
kituo kikubwa cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa madai kuwa
kituo hicho hakipokei kesi za siasa, jana walihojiwa na kutakiwa
wasubiri upelelezi utakapokamilika ndipo wataitwa tena.
Akizungumza
na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Ilala, David Mnyambuga, alisema suala
hilo halijafika kwake na kwamba ataanza kulishughulia mara baada ya
kupata maelezo ya walalamikaji hao, ambao aliwaita ofisini kwake kwa
mahojiano.
Post a Comment