Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KONDA WA DALADALA MATATANI KWA KUISHI KINYUMBA NA HUYU MWANAFUNZI HAPA!



KONDAKTA wa daladala inayopiga kazi njia ya Makumbusho na Gongo la Mboto, jijini Dar aliyetambulika kwa jina moja la Saidi (pichani), ameingia matatani baada ya kudaiwa kuishi kinyumba na mwanafunzi wa kidato cha tatu, tukio lililotokea Magomeni Kagera hivi karibuni, kinyume na sheria za nchi.


Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizo, denti huyo mwenye umri wa miaka 17 anayesoma Shule ya Sekondari Nguvu Mpya, iliyopo Chanika,  Dar aliishi chumbani kwa konda huyo baada ya bibi yake anayeishi naye maeneo ya Sinza, Dar kusafiri kuelekea Zanzibar.
Ilidaiwa kuwa wawili hao wamekuwa wakiishi kama mke na mume tokea Machi,  mwaka huu ambapo konda huyo akitoka humfungia ndani.Ndani ya chumba cha konda huyo, waandishi wetu wakiwa na polisi, walishuhudia sare za shule pamoja na begi na madaftari na katika upekuzi kwenye madaftari hayo, ilionekana mara ya mwisho aliandika Machi, mwaka huu.

Hata hivyo, kondakta huyo hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo, lakini polisi wameahidi kumsaka na kumkamata ili kumfikisha mbele ya sheria.Mwanafunzi huyo aliliambia Uwazi kuwa alikutana na konda huyo katika gari lake ambapo alikuwa akimpatia unafuu wa usafiri bila kunyanyaswa kama inavyowatokea wanafunzi wengine kabla ya kuanza uhusiano wa kimapenzi.


Alipoulizwa kuhusu wazazi wake, alidai mama yake alishafariki na hakuwahi kumuona baba yake, akidai anaishi na bibi yake maeneo ya Sinza, Dar ingawa hivi sasa amesafiri kwenda Zanzibar.

CHANZO:UWAZI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top