MAMLAKA
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imekarabati gari alilokuwa
akitumia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kutafuta uhuru kabla ya
mwaka 1961.
Gari
hilo aina ya Austin iliyotengenezwa mwaka 1947 hadi 1956 nchini
Uingereza, lilikuwa la Aminadabu Solomon Nkya ambaye alimpa Nyerere
kutembelea kudai uhuru.
Akizungumza
katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba, Mkufunzi wa Chuo cha
VETA mkoani Kilimanjaro, Hurbert Makundi, alisema chuo hicho
kimekarabati gari hilo kwa lengo la kumuenzi Nyerere aliyekifungua mwaka
1984.
Alisema
wamelikarabati gari hilo lililokuwa limekufa kabisa na kutelekezwa
katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana kazi iliyofanyika
kwa miezi sita na kurudi katika hali ya kawaida na sasa linawaka.
Alisema
baada ya maonesho wanatarajia kulikabidhi serikalini kupitia CCM Mkoa
ili kulihifadhi kama kumbukumbu, huku wakitarajia kukarabati lingine
ambalo nalo lipo mkoani humo.
Gari
hilo limekuwa kivutio kwa watu wanaotembelea banda hilo na maonesho kwa
ujumla kutokana na muundo wake wa kizamani, lakini sasa linaonekana
kuwa jipya.
Baadhi
ya wananchi waliotembelea maonesho hayo wameomba Serikali kulipeleka
gari hilo katika Makumbusho ya Taifa kama yalivyowekwa mengine.
Mwananchi
Gasper Mlay alisema gari hilo la kipekee ambalo huwezi kukutana nalo,
kupelekwa makumbusho ya Taifa kutafanya vizazi vijavyo kupata mafunzo ya
magari aliyotumia Mwalimu.
Post a Comment