Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi na ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Nazar Nyoni (84), amekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Nyoni
ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu katika Serikali ya Awamu
ya Kwanza, alisema ameamua kujiunga na Chadema baada ya kuvutiwa na
maneno ya wabunge waliomaliza muda wao, Tundu Lissu na Halima Mdee.
Alikuwa
akizungumza mbele ya viongozi wa Chadema Wilaya ya Morogoro Mjini,
wanachama na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha
wagombea ubunge na udiwani wa Jimbo la Morogoro Mjini.
Nyoni
alisema licha ya kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na kiongozi
serikalini tangu mwaka 1975 hadi 1994 huku akiwa na kadi mbili ya Tanu
na CCM, amemua kujiunga na Chadema pia baada ya kufuatilia mambo mengi
ya msingi ikiwamo Bunge la Katiba na Bunge na kutambua kuwa chama kimoja
chenye umoja na mbinu moja ni Umoja wa Katiba wa Wananchi (Ukawa).
"CCM
kwa sasa imechoka na kubaki kula fedha za nchi na kwa msingi huo,
nikiwa mzee, nimeamua kuhamia Ukawa ili niseme kabla sijaaga dunia kuwa
hakuna chama kinachoweza kuongoza Tanzana kwa sasa zaidi ya Chadema ama
Ukawa," alisema Nyoni.
Awali,
mtia wa kugombea ubunge Jimbo la Morogoro Mjini kupitia Chadema, Marcos
Mgweno, aliwaasa wana-Morogoro kuukataa unyonge walionao kwa sasa kwa
kuichagua Chadema kwa ajili ya maendeleo yao.
Mgweno
alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tajiri duniani lakini utajiri huo
hauwanifaishi wananchi husika bali wachache kwa manufaa yao binafsi.
Naye
Katibu wa Chadema Wilaya Morogoro Mjini, Esther Tawele, aliwataka
wakazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla, kutambua kuwa hatma ya maisha
yao ipo mikononi mwao hivyo ni nafasi yao kutumia Ukawa katika
kuwaletea mabadilko.
Post a Comment