1. KATIBU MKUU AKIWASALIMIA WANANCHI WA IRUGWA.
    KATIBU MKUU AKIWASALIMIA WANANCHI WA IRUGWA.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amehitimisha ziara yake ya nchi nzima kwa mafanikio makubwa. Ziara hiyo imekiwezesha Chama kuona mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika utekelezaji wa Ilani. Pia Chama kimebaini mapungufu katika utekelezaji huo wa Ilani na kimeielekeza Serikali yake kuyapatia ufumbuzi mapungufu hayo. Yapo mambo ambayo kupitia ziara hiyo, yamepatiwa majawabu na mengine ambayo hatua za ufumbuzi wake zinaendelea kuchukuliwa.
    Kutaja mifano michache tu ni pamoja naifuatayo;


    1. Migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini; Wakulima na wafugaji dhidi ya Hifadhi na wawekezaji na ya mipaka
    2. Migogoro ya wakulima na wawekezaji; mfano kiwanda cha chai Mponde
    3. Vikwazo mbalimbali katika maendeleo ya sekta ya madini,kilimo,ufugaji na uvuvi ikiwa ni pamoja na; kero zinazowakabili wakulima, wafugaji na wavuvi katika kufanikisha ustawi na maendeleo yao na nchi kwa ujumla
    4. Miradi mbalimbali ya kiuchumi na ya huduma za jamii iliyokuwa imekwama inaendelea kupatiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na ile ya maji, umeme na mawasiliano
    TAKWIMU ZA MAMBO YALIYOFANYIKA


    1. Kwa ujumla Katibu Mkuu, pamoja na msafara wake amesafiri umbali wa jumla ya Kilomita 193,537kwa gari katika mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar, ikiwa ni pamoja na Kilomita 1,510alizosafiri kwa basi kutoka Dar es Salaam hadi Bukoba. Amesafiri masaa 84 kwa njia ya maji kwa mitumbwi katika visiwa 16 nchini.
    2. Ametembelea jumla ya Mikoa 31,Wilaya mia moja sitini na tatu (163) na Majimbo yote mia mbili thelathini na tisa (239) ya uchaguzi na Kata/Wadi 1,938 nchini.
    3. Amehutubia jumla ya mikutano 1,918 ikiwemo mikutano 249 ya ndani na mikutano 1,669 ya hadhara.
    4. Amekagua, amechangia,amehimiza na kushiriki katika kazi za utekelezaji wa ilani kwenye jumla ya miradi 2,671 ikiwemo 284 ya Chama na 2,387 ya Maendeleo ya wananchi.
    5. Amepokea jumla ya wanachama wapya wa CCM 208,430 wakiwemo wanachama 36,984 kutoka vyama vya upinzani.