Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

January amvaa Lowassa


January Makamba
Aliyekuwa mgombea Urais wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Januari Makamba, jana alimshukia mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa, Edward Lowassa kwamba ni mroho wa madaraka.
Makamba alitoa kauli hiyo katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma wakati akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde. January alisema kuwa Lowassa ameivuruga demokrasia ndani ya Chadema na kupeleka mizengwe itakayokiua chama hicho na umoja wao.
“Yale siyo mabadiliko kama wanavyojinadi bali ni uroho wa madaraka kwa mtu mwenye uroho na chama chenye uroho, lakini hawezi na hawawezi kushika madaraka ya kuongoza nchi,” alisema Makamba.

Alisema kinachoendelea kwa vyama vinavyounda Ukawa ni maigizo na siyo mabadiliko ya kweli kwa sababu mgombea urais ametoka CCM na Sera za CCM na mgombea mwenza ametoka CUF na sera za huko, hivyo hawawezi kuungana kwa pamoja kwa sababu hawajui nini maana ya kile wanachogombea.
Hata hivyo, Makamba alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu kuliko uchaguzi wowote uliowahi kutokea katika mfumo wa vyama vingi na akawataka wana CCM kujiandaa kikamilifu.
Alisema CCM kinapaswa kuwa makini na imara wakati wote ili kutoyumba na wakifanya hivyo watajikuta wanapata mchanganyiko ambao utaleta shida katika maendeleo.
Kwa upande wake mgombea ubunge Mavunde alijipachika jina la Mr Makao akisema lazima ataipelekea Dodoma hadhi ya kweli katika kufikia makao ambayo yamekuwa yakisemwa kama hisani.
Mavunde aliomba wananchi kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwani ana uhakika kwa miaka mitano ataifanya Dodoma kupaa kiuchumi huku akisema atashughulika na watu wenye kipato cha chini pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi.
Chanzo:Mwananchi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top