Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Lowassa AFUNIKA Iringa ..... Aendeleza dozi nzito ya UKAWA kwa CCM

Waziri wa muda mrefu wa Elimu Joseph Mungai na mkewe wamekihama Chama cha Mapinduzi na kujiunga na Chadema huko Mafinga leo.

Hii ni baada ya Mgombea Urais wa Ukawa Edward Lowassa kuingia Iringa leo


Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema amechoshwa na manyanyaso wanayoendelea kuyapata wakulima hapa nchi kwa kukopwa mazao yao na kutozwa ushuru na serilkali bila ya wao kupata faida yoyote.

Lowassa alisema punde atakapochaguliwa kuongaza nchi kitu kikubwa atakachokifanya kuwasaidia wakulima ni kufuta ushuru wote wa mazao kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho wanalolitoa wakati wa kilimo.

Lowasa ameyasema hayo leo wilayani Mufindi alipofanya mkutano wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Wambi, mjini Mafinga.

Lowassa alisema watu wamekuwa wakizungumza kuwa CCM ni wezi wa kura kwasababu ni wajanja sana katika kufanya michezo michafu katika chaguzi na maneno hayo si yakuyabeza wala kuyafumbia macho.

“Mimi nataka kila mtu akihifazi vizuri kichinjio chake (kadi ya kupigia kura) na siku ya kupiga kura ikifika nawaomba wanawake na wanaume wajitokeze kwenda kupiga kura ila wakina baba nawaomba mkishapiga kura fanyeni kazi ya kuzilinda kura zenu” alisema Lowassa

Katika mkutano huo, waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai alipanda jukwaani na kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini kupitia Chadema, William Mungai ambaye ni mtoto wake.

Mungai aliwahi kuwa mbunge kwa miaka 35 kupitia CCM na aliweza kuteuliwa nafasi mbalimbali za uwaziri ikiwamo Wizara ya Kilimo, Mambo ya Ndani na Wizara ya Elimu.

Mungai alisema wananchi wa jimbo hilo wanatakiwa kumchagua William Mungai kwa sababu mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo hilo hakuweza kuongoza kama alivyofanya yeye.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top