Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZEE WA KARATU WAMUITA DKT. SLAA...........WAMPA WOSIA MZITO,HEBU WASIKIE

Na Mwandishi Wetu
WAKATI vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kesho vitazindua kampeni zake za urais kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu kwenye Viwanja vya Jangwani, Dar, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa ameitwa na wazee wa nyumbani kwao, Karatu mkoani Arusha, Uwazi Mizengwe limedokezwa.

Chanzo kilicho karibu na kiongozi huyo mwenye mvuto na ushawishi kisiasa ambaye kwa sasa yupo katika ‘mgogoro’ na chama chake, kimesema Dk. Slaa aliitwa ili kuweka mambo sawa kufuatia sintofahamu inayoendelea kati yake na viongozi wenzake wa Ukawa tangu ujio wa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Edward Ngoyai Lowassa ambaye ni mgombea wa urais kupitia Ukawa.

Inadaiwa kuwa baada ya kuwa kimya kwa wiki kadhaa akiwa nyumbani kwake Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kiongozi huyo alikerwa na wageni wa aina mbalimbali waliokuwa wakifika nyumbani kwake kwa kupishana, wengi wao wakienda kwa lengo la kumshawishi ili atangaze uamuzi wake kuhusu siasa kitu ambacho hakuwa tayari kukifanya kwa wakati huo.

MANENO YA CHANZO
“Kama wiki mbili mbili zilizopita, Dk. Slaa aliondoka Dar es Salaam kwenda mapumzikoni katika Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Mara ambako aliandamana na familia yake.”

Mizengwe: Samahani. Unaposema aliongozana na familia yake, una maana na mkewe, Josephine?”

Chanzo: “Mimi sijui hilo. Elewa alikwenda na family yake. Lengo la safari yake ni kupata nafasi nzuri ya kutafakari mustakabali wa maisha yake kisiasa. Hapa Dar aliona anakosa utulivu kutokana na kupata wageni mara kwa mara. Wanaingia na kutoka.”


Mizengwe: “Ni akina nani? CCM, Chadema, Ukawa au ndugu, jamaa na marafiki?”

Chanzo: “Sijui…sijui! Sasa akiwa kule, wazee wa nyumbani kwao (Karatu) wakasikia, wakaona ni wakati muafaka kwao kumuita na kuweza kuzungumza naye ili kwanza wajue msimamo wake, lakini pia waone kama wanaweza kumshauri lolote la kufanya katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia katika uchaguzi mkuu na kampeni zimeshaanza.”


BADO YUPO KARATU
Inadaiwa kuwa kwa zaidi ya wiki moja sasa, Dk. Slaa yupo Karatu ambako mazungumzo kati yake na wazee wa huko yanaendelea. Upo uwezekano mkubwa wa kutokuwepo jijini Dar (kesho) wakati Ukawa watakapoanza kampeni zao kumnadi mgombea wa urais ambaye ni Lowassa.


WAZEE WAGAWANYIKA
“Lakini kinachoonekana ni kwamba, hata kule nyumbani kwao nao wazee wamegawanyika. Wapo wanaomtaka dokta ahamie CCM na wengine wanamtaka kurejea kuendelea na harakati za kuijenga Chadema. Lakini hadi hapa ninapozungumza na wewe, bado hakuna uhakika juu ya uamuzi wa Dk. Slaa.” Chanzo.


Chanzo kikaendelea kudai kuwa, wazee hao walimwambia maisha yake ni ya siasa hivyo kujitenga kwake kunaweza kuirudisha nchi katika enzi zisizokuwa na ushindani wa vyama vingi. Walimwambia atafakari upya kwa sababu kuwa kwake nje ya Chadema kuna msururu wa watu wengine nyuma yake.

DOKTA KIMYA
Kikaendelea: “Lakini dokta kama kawaida yake. Bado hasemi chochote, yeye si mtu wa kukurupuka. Si unamjua! Hajatoa jibu.”


UKAWA JANGWANI
Wakati huohuo, kesho Ukawa watazindua kampeni zao kwenye Viwanja vya Jangwani huku viongozi wawili waandamizi na waanzilishi wakiwa wamejiweka kando.


Viongozi hao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba aliyejiuzulu nafasi hiyo wiki chache zilizopita na Dk. Slaa. Wote wakidaiwa kutoridhishwa na mchakato wa kumkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kisha kupewa nafasi ya kugombea urais.

WITO WA DK. SLAA
Tangu Dk. Slaa ajiweke kando, maneno mengi yamekuwa yakisemwa kuhusu padri huyo wa zamani, lakini mara zote amewataka Watanzania kuwa wavumilivu kwani wakati muafaka ukifika, ataeleza kilichomo moyoni mwake.


Uwazi Mizengwe juzi lilimtafuta Dk. Slaa kwa njia ya simu bila mafanikio. Hata lilipofika nyumbani kwake, mwenyeji mmoja aliyegoma kujitambulisha, alisema kiongozi huyo yupo nje ya jiji kwa shughuli zake binafsi.

chanzo:uwazimizengwe
- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/08/wazee-wa-karatu-wamuita-dkt-slaa.html#sthash.garPpqP2.dpuf
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top