Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHADEMA YAIBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI ...

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Lameck Mlacha, ametupilia mbali mapingamizi yaliowekwa na RPC wa Mwanza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa mleta maombi ambae ni Baba mdogo wa Mawazo hana uhalali wa kisheria wa kuleta maombi hayo kwa kuwa yeye si baba mzazi wa marehemu, na kuwa hajaleta hoja za kubishaniwa kwenye maombi hayo.

Upande wa utetezi unaoongozwa na mawakili John Mallya, James Millya na Paul Kipeja ulijibu hoja hizo kuwa katika hatua hiyo masuala ya kubishaniwa hayana sababu ya kuletwa kwa kuwa ni hatua ya awali sana.

Kuhusu uhalali wa kisheria wa baba mdogo wa marehemu, majibu yalikuwa kwamba baba mdogo kwa kuwa ndiye aliemlea Marehemu Mawazo, anayo mamlaka na uhalali wa kisheria wa kuleta maombi hayo.
Mahakama imekubaliana na hoja za mawakili wa mleta maombi na kuamua kuruhusu kesi ya msingi kufunguliwa kama ilivyoombwa, na kutupilia mbali mapingamizi ya RPC na AG.
Upande wa wapeleka maombi utawasilisha maombi ya kesi ya msingi leo hii mchana, kisha tutasubiri maelekezo ya Mahakama kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa lini!
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top