Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Matumizi ya TEHAMA yaboresha ufanisi Serikalini.



Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA katika kufanya mikutano kwa kutumia mfumo wa Mawasiliano ya (Video comference) ambapo kikao kimoja kitawaunganisha pamoja washiriki kutoka Mikoa 8 ambapo mada huwasilishwa na kutoa fursa ya kuwasiliana moja kwa moja (interactivity) kwa maswali na ufafanuzi leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kati ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es asalam.Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA katika kufanya mikutano ambapo mfumo wa Mawasiliano ya (Video comference) utatumika ili kupunguza gharama za mikutano kwa Taasisi za Serikali.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu faida za kutumia TEHAMA ikiwemo kuokoa fedha zilizokuwa zinatumika awali kuandaa mikutano hiyo ambapo kwa sasa washiriki watashiriki mikutano hiyo wakiwa katika vituo vyao vya kazi leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango. (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)


..…………………………………………………………………………………………

Na Jovina Bujulu-MAELEZO
Uanzishaji wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini utaboresha na kuongeza ufanisi wenye tija ambao utapunguza gharama za utendaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. 


Kupitia utaratibu huu wa vikao kazi ambavyo vitaendeshwa kwa kutumia mfumo wa mawasiliano ya video ambapo kikao kimoja kitaunganisha kwa pamoja washiriki kutoka mikoa nane ambapo mada huwasilishwa na kutoa fursa ya kuwasiliana moja kwa moja kwa maswali na ufafanuzi. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu matumizi ya TEHAMA katika kupunguza gharama za uendeshaji vikao kazi. 

Mfumo wa mawasiliano ya video ni teknolojia inayowezesha mawasilano kutoka vituo mbalimbali kuwasiliana kwa njia ya sauti na picha kwa njia ya kielekroniki bila kuhitaji kukutana eneo moja. 

“Teknolojia hii ya kutumia mfumo wa mawasiliano ya video itapunguza gharama mbalimbali za uendeshaji vikao Serikalini ambazo ni pamoja na kukodi kumbi za mikutano, usafiri na muda ambao hutumika nje ya vituo vya kazi” alisema Temba. Aidha, Bw. Temba alisema kuwa utaratibu wa vikao ni rasmi kama ilivyo mikutano mingine ya kazi ambao ni salama kwa kuwa miundo mbinu yake inaratibiwa na Serikali. 

Bw. Temba aliendelea kusema kuwa mwongozo wa mawasiliano kwa njia ya video umetolewa na unapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, “Mwangozo huu unahusu wajibu wa Wizara, idara, Wakala za Serikali na Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika kuboresha mawasiliano kwa njia ya video” aliongeza Bw.Temba  Pia mwongozo huo unaainisha mazingira na vifaa ya kuendesha mawasiliano kwa njia ya video kuzingatia sifa na viwango vya chini na kuhakiki mfumo huo kabla ya matumizi. 

Mfumo huo ulianzishwa na Serikali mwaka 2013/2014 katika mikoa ya Kilimanjaro, Kagera, Morogoro na Iringa kati ya utumishi na mamlaka za Serikali za mitaa ambapo kwa sasa mawasiliano hayo yanapatikana nchi nzima isipokuwa mikoa mipya ya Geita, Simiyu, Katavi na Njombe.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top