Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Baraza la Mawaziri la Magufuli ni Balaa......Yadaiwa Kila Waziri Atatia Saini Kukubali Masharti Yaliyowekwa na Magufuli



Kusuasua kwa Rais John Magufuli, kutangaza Baraza la Mawaziri kunatokana na msimamo wake wa kuwachambua watu anaotarajia kuteua katika nafasi hiyo huku akiaandaa mikataba ya makubaliano itakayokuwa mwongozo kwa mawaziri hao.

Nia ya Rais, hadi kufikia hatua hiyo imetafsiriwa kwamba anataka kupata mawaziri ambao wataweza kwenda sambamba na kasi yake pamoja na wawajibikaji.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaeleza kwamba kwa sasa Rais Magufuli, anasuasua kutangaza baraza lake kutokana na kile kinachodaiwa ni kuandaa mikataba ambayo mawaziri baada ya kuteuliwa watalazimika kuisoma kwa muda wa siku mbili kabla ya kukubali uteuzi huo.

Chanzo hicho, kilieleza kwamba wale watakaokubali itabidi wasaini mkataba huo ili kukukabiliana na matakwa ya  mkataba huo.

“Kwa sasa huyu jamaa anaandaa mikataba kwa ajili ya kuwapatia Mawaziri na Manaibu wake na wanatakiwa kuisoma ndani ya siku mbili na yeyote atakayekubaliana na mkataba huyo atalazimika kuisaini.

“Mikataba ya Mawaziri na Manaibu inalenga kuwabana watumishi hao na kukubaliana kuwa iwapo itatokea tatizo katika wizara husika wao watakuwa wa kwanza kuwajibishwa.

“Mkataba unalenga kuwafanya Mawaziri hao na Manaibu wao kuhakikisha wanafanya kazi kwa uaminifu, uadilifu, na kwa kujali maslahi ya jamii,” kilisema chanzo hicho.

Pia kilisema mkataba huo unaonekana unamasharti kwamba endapo siku mawaziri hao watajiingiza kwenye vitendo vya kifisadi au Wizara husika kulaumiwa watalazimika kujiuzulu bila kubembelezwa huku mhusika akifishwa kwenye vyombo vya sheria bila mjadala.

Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa kwa sasa wabunge waliowengi wanaogopa nafasi za uwaziri na unaibu kwa madai kuwa kasi ya Rais Magufuli ni kubwa na inaweza kumtia hatiani mtumishi wakati wowote.

“Wabunge hao wanapata homa kubwa kutokana na hatua ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa kuonesha ushujaa wa ajabu kwa kuwashambulia vigogo ambao wameshindikana katika vitendo vya ukwepa wa ulipaji kodi au kufanya ubadhilifu katika maeneo mbalimbali ikiwemo bandari.

“Kitendo kinachofanywa na Rais Magufuli ni sawa na kumvua nguo Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) kwani kwa madudu ambayo yanaonekana inaonesha wazi kuwa nchi haikuwa na kiongozi na kama ilikuwa na kiongozi basi kiongozi huyo alikuwa na mkono wake.

“Sikiliza kijana haiwezekani nchi ikawa na wafanyabiashara wakubwa na matajiri wakubwa wanaokwepa kodi huku kiongozi wa nchi kwa kujua ama kutokujua anakaa nao meza moja kwa kuwapongeza kwa misaada kiduchu wanayotoa katika jamii huku wafanya biashara hao wakiongeza wigo waliyonacho na wasiyonacho jambo ambalo ni hatari,” kilisema.

Wakati huo huo kuna tetesi kuwa kutokana na kasi ya Rais Magufuli kwa sasa ndani ya CCM kuna mvutano mkubwa ambapo wanataka kubadilisha katiba ya chama hicho.

Mgongano uliopo kwa sasa ndani ya Chama ni kutaka kubadilisha katiba ya chama hicho ili rais asiwe mwenyekiti wa chama.

“Hofu hiyo inatokana na kasi ya Rais Magufuli na inasemekana akiwa mwenyekiti watendaji wote ambao wapo maofisini kihasara hasara watakuwa na wakati mgumu zaidi.

“Mbali na hilo kwa sasa inaonesha wale watu ambao walikuwa wanapatiwa madaraka kwa njia ya kulindana itakuwa hadithi kwani waliowengi wanaweza kutimliwa,” kilisema chanzo hicho.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top