Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BARAZA LA WAFANYAKAZI MUHIMBILI LAZINDULIWA

atibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu wa baraza hilo, Dk Kissa Mwambene. Kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakipiga makofi wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya wakizungumza na wajumbe wa baraza hilo Leo kwenye hospitali hiyo.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi LEO kabla ya kupiga kura za kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani wa hospitali hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la MNH wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru katika kikao hicho.
Wajumbe wakipiga kura LEO za kuwachagua viongozi wapya wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali hiyo.
Dk Kissa Mwambene akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua Leo kuwa Katibu wa baraza hilo.
Wakili Eneza Msuya akiwashukuru LEO wajumbe baada ya kumchagua kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.
Kutoka kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dk Kissa Mwambene, Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Lawrence Museru, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu Msaidizi wa baraza hilo, Wakili Eneza Msuya na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha maslahi ya watumishi wake na kuendelea kuweka miundombinu bora ya kiutendaji.Akizindua Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dk. Ulisubisya amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa kwani inampa motisha mtumishi kufanya kazi kwa bidii.

“Nimefarijika sana kuoana suala la maslahi ya watumishi linapewa kipaumbele hapa MNH kwa kweli mnastahili pongezi na taasisi nyingine hazina budi kuiga mfano huu, lakini napenda kusisitiza kuwa kila mtumishi ni vema akanufaika na maboresho haya amesema,” Dk Ulisubisya.Akizungumza kabla ya uzinduzi wa baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema hivi sasa hospitali hiyo imeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 2 hadi kufikia Bilioni 4.
Pia amesema katika kuendelea kuboresha huduma za matibabu MNH ina mpango wa kuongeza ICU ya watoto wadogo pamoja na ICU ya kina mama wenye matatizo ya uzazi ili kuokoa maisha ya mama na mtoto .Kwa mujibu wa Profesa Museru Hospitali hiyo ipo katika hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkopo ambao utasaidia kupanua huduma za afya ikiwamo kununua vifaa tiba vya upasuaji.

Katika kikao, wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wamemchagua Dk. Kissa Mwambene kuwa Katibu wa Baraza hilo pamoja na Eneza Msuya kuwa Katibu Msaidizi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top