Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATU TISA MBARONI KWA KUUZA SUKARI KINYUME NA BEI ELEKEZI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo. 

Arusha. Polisi mkoani Arusha inawashikilia watu tisa kwa kosa la kuuza sukari tofauti na bei elekezi ya Sh1,800.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema leo kuwa watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na watashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Mkumbo alisema mmoja wa watu hao amekutwa akiuza kwa Sh5,000 kwa kilo moja.

Alisema wengine walikamatwa wakiuza sukari Sh6,200; Sh3,000; Sh2,500  na Sh4,500 kwa kilo.

Kamanda Mkumbo amesema kamatakamata ya watu wa aina hiyo ni endelevu na aliwashauri wafanyabiashara wote mkoani Arusha kuuza sukari kwa bei elekezi iliyopangwa na Serikali.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top