Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BUNGENI HAPAKALIKI ... WABUNGE WENGINE WASIMAMISHWA KUHUDHULIA VIKAO VYA BUNGE


Leo June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Sika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest.

Mbunge Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni Idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.

Aidha Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top