Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHINA KUFADHILI UCHAPISHAJI WA VITABU MKOA WA DAR

SERIKALI ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Jimbo la Jiangsu imetoa fursa ya kufadhili uchapishaji wa vitabu milioni 1.4 vya masomo ya Sanaa na Biashara kwa ajili ya Shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uwekaji saini ya hati ya makubaliano kati ya mkoa wa Dar es Salaam na Jimbo la Jiangsu la nchini China, Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amewashukuru kwa ushirikiano na kuonesha kusaidia sekta ya elimu nchini inayokabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ukosefu wa vitabu.

Alisema vitabu hivyo vitakavyochapishwa ni vipya kabisa na kwa mara ya kwanza vitaanza kutumika katika shule za Dar es Salaam.

“Nina imani kwamba leo ni mwanzo wa kushirikiana kwa karibu ili kuvutia shughuli nyingi zaidi za kushirikiana kati ya sekta za umma na za binafsi zilizoko katika maeneo yetu ikiwemo ajira kwa vijana, mazingira, ufadhili wa masomo China, afya ya mama na mtoto pamoja na uwekezaji katika sekta ya viwanda,” alisema Makonda.

Aidha, amewakaribisha kuja kuwekeza nchini hususani Dar es Salaam akisema Tanzania ina fursa za uwekezaji katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na biashara, ujenzi wa majengo kwa matumizi ya makazi na biashara, barabara, elimu, afya, udhibiti wa taka ngumu, usafiri mjini, utalii na viwanda.

Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Wananchi wa Jimbo la Jiangsu, Luo Zhijun alisema, China na Tanzania zimekuwa zikishirikiana kwa muda mrefu hivyo kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano ni mwendelezo wa kudumisha uhusiano.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top