Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JESHI LA POLISI LAWAGEUKIA WENYE NYUMBA NA WAPANGAJI WA NYUMBA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wenyeviti wa serikali za mitaa kushirikiana na wenye nyumba kuhakikisha wapangaji katika nyumba wanaingia makubaliano ya mkataba na kuwa na picha zao.
 
Hatua hiyo imetokana na kuwepo kwa watu wanaofanya uhalifu katika maeneo mbalimbali na kushindwa kupatikana pindi polisi wafanyapo operesheni kutokana na kupanga kwenye nyumba hizo lakini wakati akiondoka hawaagi na wenye nyumba wanakosa kuwa na taarifa za watu katika nyumba zao.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa wenye nyumba ambao watashindwa kufanya mkataba bila picha likitokea tukio dhidi ya mpangaji msalaba utamuangukia mwenye nyumba kuhusika katika uhalifu uliofanywa.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi linamshirikia Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), MT 66807 SGT, George Kwisema kwa tuhuma za kukutwa na vipande kumi vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh. milioni 198 vikiwa katika gari yake yenye namba za usajili T.477 AXS aina ya Suzuki Vitara.

Katika tuhuma za vipande vya meno ya tembo wanaoshikiriwa wengine, ni Shafi Muhibu pamoja na Asha Hassan ambao walikutwa katika gari iliyokuwa imebeba meno ya tembo.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi linawashikiria watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na sukari mifuko 35 ya Kilogram 50 ambao walikamatwa Chadibwa Mtaa wa Magogoni Kigamboni Mei 31 mwaka huu, ambayo ilikuwa haijalipiwa ushuru na waliokamatwa na tuhuma za sukari ni Said Bakari (25), Mkazi wa Mbagala , Hamadi Selemani pamoja na Bakari Masudi.

Jeshi la Polisi linafanya upelelezi pia wa mtuhumiwa wa aliyewaleta wahamiaji Haramu na kutoweka katika mazingira ya utatanishi akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top