Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKINDA AIBUKIA MAKAO MAKUU NHIF

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda (kushoto) akiwasili kwenye Makao Makuu ya NHIF kwa siku ya kwanza mara baada ya kuteuliwa na kuwa mwenyekiti wa bodi wa mfuko huo leo jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamoto pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti. Mh. Makinda alipata, pia fursa ya kuwa na mazungumzo mafupi na uongozi wa Mfuko huo chini ya Kaimu Mkuu wake, Bernard Konga na vilevile alitembelea baadhi ya ofisi ikiwemo kituo cha utunzaji nyaraka za mfuko kwa njia za kielektroniki, kituo cha huduma kwa wateja na kituo cha utunzaji taarifa za Mfuko kwa lengo la kuona jinsi zinavyofanya kazi leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda akiwa katika chumba maalum cha kuhifadhi nyaraka mbalimbali za wanachama wa mfuko huo leo mara baada ya kufanya ziara kutembelea Makao Makuu ya Mfuko huo leo jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda akionyeshwa sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu za wanachama mara baada ya kufanya ziara kutembelea Makao Makuu ya Mfuko huo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda akipata maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika Mstaafu, Mama Anne Makinda akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa NHIF, Bernad Konga mara alipofanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya NHIF ya Kurasini leo jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo fupi ya utambulisho
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akimpa taarifa Mwenyekiti wa Bodi Mpya wa NHIF, Spika Mstaafu, Mama Anne Makinda mara alipofanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya NHIF ya Kurasini leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Mfuko huo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top