Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MANISPAA YA KINONDONI HAPAKALIKI .... TIMUA TIMUA YAZIDI KUSHIKA KASI

 Meya wa Halmashauri ya Manispaa Kinondoni  Boniface Jacob  akizungumza na  Mafisa Watendaji  juu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  na kuwafukuza kazi mafisa watendaji kata wawili kutokana ubadhirifu fedha za umma.

HALMASHAURI ya Manispaa ya kinondoni imefukuza kazi mafisa watendaji kata wawili kutokana ubadhirifu fedha za umma.

Akizungumza leo na maafisa watendaji kata, meya wa kinondoni boniface jacob amesema kuwa hawatavumilia  watendaji wanaofuja fedha za umma.

Watendaji waliofukuzwa ni Ernest Misa na Ally Bwanamkuu na wengine wawili wamesimamishwa kazi kwa uchunguzi ambao ni Shaban Kambi pamoja na Bernard Supu.

Aidha Meya huyo amesema zipo kata tano ambazo zimekusanya mapato vizuri na kata tano zingine zimefanya vibaya hivyo wanatafuta dawa ya kuwaondoa watendaji waliofanya vibaya.

Jacob amesema migogoro ya ardhi imepungua kutokana na kila watendaji kuwajibika katika zao awali migogoro ilikuwa inasababishwa na wenyewe

Amesema kinondoni wanataka kuibadili katika kuhakikisha watendaji wanawahudumia wananchi kuachana kufanya kwa mazoea.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top