Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAOFISA WANAOKOPA KOPA KUTIMULIWA

WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba amewaagiza wakuu wa wilaya nchini, kuwachunguza maofisa ushirika na warajisi wa vyama vya ushirika.

Lengo la hatua hiyo ni kubaini iwapo wanatumia madaraka yao vibaya, kukopa kwenye ushirika kisha kuacha deni kwa wakulima.

Alisema kuwa iwapo watabainika kufanya hivyo, wachukuliwe hatua kali za kisheria mara moja.

Alisisitiza kuwa katika uchunguzi huo, polisi ishirikishwe kwa karibu zaidi. Waziri huyo alitoa agizo hilo juzi mjini hapa wakati wa kikao chake na viongozi wa vyama vitano vya msingi vya wakulima wa tumbaku katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Alisema taarifa alizonazo ni kwamba wapo baadhi ya maofisa ushirika na mrajisi, wamekopa fedha Benki ya CRDB kwa mgongo wa vyama vya ushirika vya wakulima wa tumbaku, wakati wao hawastahili, kwa kuwa sio wakulima wala wanachama.

“Lakini kama vile hiyo haitoshi, wakopaji hao haramu hukimbia bila kurejesha fedha walizokopa na kuwaachia mzigo wakulima kulipa madeni hayo… serikali haiwezi kukubali wajanja wachache wajinufaishe kwa kutumia vyama vya wakulima. Uchunguzi wa kina lazima ufanyike na ikibainika ofisa ushirika au mrajisi amekopa na kurejesha yeye binafsi, basi huyo hana tatizo,” alisema.

Waziri Nchemba alisema kuwa kwa watakaobainika kuchukua mikopo kwa manufaa yao binafsi, kisha kukimbia deni na hatimaye mkopo kurejeshwa na vyama vya ushirika vya msingi, wachukuliwe hatua za kisheria.

Wakati huo huo, Waziri Nchemba ametangaza kufuta mara moja makato mbalimbali ya fedha ambazo wakulima wa zao la tumbaku walikuwa wakikatwa kutokana na maelezo ya makato hayo kutojitosheleza na kuwa na ukakasi.

“Kuna ujanja unatumika, maelezo ya makato haya yanaandikwa kwa kiingereza na malipo yanafanyika kwa dola za Marekani.. hii yote ni kumchanganya mkulima wa tumbaku, serikali haiwezi kukubaliana na mtindo huu,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top