Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWALIMU ADAIWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI WAKE

Shinyanga. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephina Matiro ameliagiza jeshi la polisi kumkamata aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Mwadui Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumpaa mimba mwanafunzi wa darasa la sita na kumtelekeza.

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kupinga mimba na ndoa za utotoni ulioandaliwa na shirika la Agape  linalohusika na kupinga vitendo hivyo uliofanyika mjini Shinyanga, Mtiro alilitaka jeshi la polisi kuhakikisha wanamtia mbaroni mwalimu huyo.

“Hatuwezi kuendelea kulea vitendo viovu vinavyofanywa na walimu kwa makusudi huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria, lazima tumtie hatiani ili iwe fundisho kwa walimu wengine wenye tabia kama za kwake,” alisema Mtiro.

Akizungumzia tukio hilo, mama wa mzazi wa binti huyo, Anna Masanja alisema mwanae mwenye umri wa miaka 12 amekatishwa masomo akiwa darasa la sita baada ya kupewa mimba na mwalimu huyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top