Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWEMBE WENYE TASWIRA YA NYERERE WAWA GUMZO

Mwembe wenye taswira ya sura ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

TANGA: Mti aina ya mwembe uliopo katika eneo la Tangamano ndani ya iliyokuwa karakana ya Shirika la Reli umekuwa kivutio kikubwa jijini hapa kutokana kuwa na taswira ya sura ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.'

Kumekuwa na makundi ya watu ambao wamekuwa wakifika katika eneo hilo kila siku kuutazama mti huo na kushangaa maajabu hayo.

 Wakati wa usiku mti huo unafanana kabisa na kivuli cha uso wa Mwalimu Nyerere.

Hayati  Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Habari za kuwepo kwa mti huo zilianza kuenea jijini hapa wiki moja iliyopita lakini diwani wa eneo hilo, Selemeni Musa aliliambia UWAZI aligundua mti huo ulikuwa na sura ya Mwalimu Nyerere mwezi mmoja uliopita.

 “Sikujua kama habari za mtu huo zitakuja kuwa kubwa kiasi hiki,” alisema na kuongeza kuwa watu wengi wanauchukulia mti huo una sura ya Mwalimu Nyerere baada ya kuambiwa na wengine.

 “Mtu anapokuja kuutazama tayari anakuwa na ile picha akilini ndiyo maana anaona una sura ya Mwalimu Nyerere lakini huu mti ulikuwepo hapa kwa miaka mingi,” alisema.

 UWAZI limegundua mambo matatu yaliyojificha kuhusiana na mti huo.

 Kwanza kwa mujibu wa diwani wa eneo hilo, mti huo umekuwepo kwa karibu miaka ishirini na mitano bila watu kutambua kuwa una sura ya Mwalimu Nyerere.

 Pili mti huo umeota ndani ya iliyokuwa karakana ya shirika la reli ambayo kwa sasa haitumiki tena.

 Tatu eneo hilo kwa mujibu wa maelezo ya diwani huyo ni la hatari kwa sasa kwa sababu limeota vichaka vinavyohifadhi nyoka ambao mara nyingine hufika hadi katika makazi ya watu.

 Kutokana na eneo hilo kutembelewa na watu wengi kwa sasa, diwani huyo amewataka watu wanaofika kutazama mti huo kutojiingiza kwenye vichaka hivyo kwa ajili ya usalama wao.

 Pia amelitaka jeshi la polisi kuweka ulinzi kwa ajili ya usalama wa watu wanaofika katika eneo hilo hasa nyakati za usiku.

 “Unajua watu wanakuwa wengi lolote linaweza kutokea,”  alisema diwani huyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top