Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZITTO KABWE AHOJIWA POLISI .... MAELFU WAJITOKEZA, ULINZI MKALI WAIMARISHWA

3
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-WAZALENDO), Zitto Kabwe (kulia)  akitoka katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam baada ya mahojiano.
4.Zitto Kabwe akihojiwa na wanahabari.…Akihojiwa na wanahabari.
5.Mwanasheria wake,Stephan Mwakibola akihojiwa na wanahabari.Mwanasheria wake, Stephan Mwakibola, akizungumza na wanahabari.
6.Ulinzi ukiwa umeimarishwa vya kutosha eneo hilo.
7Ulinzi ukiwa umeimarishwa vya kutosha eneo hilo.
8.Mapaparazi wakiwa kazini.Mapaparazi wakiwa kazini.
MBUNGE  wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu  chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, mapema leo aliitikia wito kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Camilius Wambura,  wa kufika katika kituo kikuu cha polisi polisi jijini Dar  alipohojiwa kwa zaidi ya saa tatu.
Akizungumza na wanahabari kituoni hapo mara baada ya kutoka, mwanasheria wake, Stephan Mwakibola, alisema kuwa  kiongozi huyo amehojiwa kuhusiana na maudhui ya hotuba ambayo aliitoa Jumapili iliyopita katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Mbagala- Zakhem jijini Dar.
Naye Zitto alisema kuwa  anasikitika kuona siku hizi kiongozi wa chama cha siasa anapokwenda kwenye mikutano analazimika afikirie kutafuta maneno ya kuzungumza.
Mwakibola alieleza kuwa polisi wamemruhusu Zitto kuendelea na shughuli zake za kila siku baada ya kupewa dhamana, na Jumatano ijayo ametakiwa kuripoti tena  polisi.  Hata hivyo,  wakili huyo hakuwa tayari kuweka bayana sehemu ya hotuba ambayo ililileta utata kwa sababu  suala hilo bado liko chini ya upelelezi.
NA DENIS MTIMA/GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top