Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BINGWA WA KUBIKIRI WATOTO AKAMATWA

 Aniva amekuwa akilipwa kuwabikiri watoto

Raia mmoja wa Malawi alionekana katika habari moja ya BBC akihusishwa na tambiko la usafishaji wa wasichana wadogo kupitia kushiriki ngono nao amekamatwa.

Eric Aniva amekamatwa kufuatia agizo la Rais Peter Mutharika kulingana na mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya rais Bright Molande aliyezungumza na BBC.

Amesema kuwa Bw. Aniva aliyepewa jina la utani kuwa 'fisi' kwa jukumu lake katika uovu huo atashtakiwa kwa kukiuka haki za watoto.
Aniva

 Pia amesema kuwa rais amechukizwa na yaliofichuliwa katika habari hiyo na ameapa kukabiliana na tamaduni hiyo.
Mtu aliyetajwa katika habari hiyo ambaye alifanya mapenzi na zaidi ya wasichana 100 pia imebainika kuwa alikuwa na virusi vya ugonjwa wa ukimwi.

Tamaduni hiyo ya usafishaji ilipendekezwa na kufadhiliwa na baadhi ya jamii kusini mwa Malawi lakini serikali imejaribu kuisitisha.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top