Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWS... LOWASSA APINGA OPERESHENI YA UKUTALeo Tarehe 31/7/2016 mjumbe wa halmshauri kuu ya chadema na mgombea wa kudumu wa chama hicho mh Lowassa amesema haungi mkono hatua zinazotaka kuchukuliwa za kuitisha maandamano nchi nzima badala yake anapendekeza pande zote mbili Serikali na Upinzani wakea wazungumze.

Akizungumza kwenye mahojiano katika kipindi maarufu cha Azam TV kinachoendeshwa na Tido Mhando Mh Lowassa aliyasema hayo baada ya kuulizwa swali lililomtaka atoe mtazamo wake kuhusu msuguano wa kisiasa uliopo nchini kwa sasa hasa hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na Chadema kuandamana nchi nzima.

Mh Lowassa alisema yeye anaamini katika mazungumzo na hakuna kinachoshindikana kwenye mazungumzo kama wakiamua huku akimalizia kwa kusema amani tuliyo nayo hapa nchini ya kuilinda kwa nguvu zote.

Kauli hii inakwenda Sambamba na kauli ambayo amewahi kuitoa siku za nyuma za kukinyima Chadema kuachana na siasa za uana harakati na badala yake wajikite kujipanga kuchukua Dola. Leo amerudia tena kwa kusema haamini sana kufanya siasa za unanaharakati na Muda sasa umefika wa Chadema kuivuka stage hiyo ya uanaharakati na kukomaa kuitafuta Dola. Lowassa amedai kuwa siasa za uanaharakati ni stage za kwanza kabisa za chama kinachokua  tafsiri inayotupa mtizamo kuwa bado chadema hakijakuwa kwa kuwa bado wapo kwenye stage za mwanzo.

Swali kuhusu kashfa ya Richmond Lowassa amedai kuwa hatakaa alizungumzie tena sakata hilo kwa kuwa ni miaka kumi sasa kila siku linazungumziwa. Aidha amedai kuwa alionewa kwa kutokupewa muda wa kujitetea. Hii ni mara nyingine tena Lowassa anashindwa kulielezea sakata lile pamoja na kuwa mara kwa mara amekuwa akipata platform ya kutoa utetezi wake kama kipindi cha nyuma alinyimwa fursa hiyo jambo ambalo linazidi kuweka sintofahamu ya uhusika wake kwenye kashafa ile. Hata hivyo amedai kuwa Sakata la Richmond limekuwa likitumiwa na baadhi ya wanasiasa kupata vyeo.

Alipoulizwa uhusiano wake wa kirafiki na Jakaya Kikwete amedai hana mgogoro wowote na JK japokuwa ni muda mrefu hawajaonana naye. Kwa maana hiyo urafiki wake upo pale pale.

Swali lingine aliloulizwa lilikuwa ni kuhusu hatua za serikali kuahamia Dodoma yeye analitazamaje. Akijibu Swali hilo Lowassa amedai kuwa serikali za awamu zote zimekuwa na malengo hayo ya kuhamia Dodoma sema mambo huingilia maamuzi hayo na hatimaye kushindwa kukamilika. Anadai yeye anaunga mkono hatua zinazochukuliwa na mh Magufuli za kuihamishia serikali Dodoma ila amemtaka kuchukua tahadhari wasije wakasababisha matatizo mbeleni.

Kuhusu vipaumbele vya rais Magufuli yeye anavionaje kwa yale ambayo ameshayafanya Mh Lowassa amempongeza Mh Raisi kwa yote aliyoyafanya ila amepingana naye kwa namna alivyoshughulika na swala la Madawati. Mh Lowassa amedai kuwa angelikuwa ni yeye asingelianza na swala la madawati kwanza kwenye elimu badala yake angejikita kuboresha maslahi ya waalimu, kuondoa upungufu wa madawati na mwishoni angelishughulikia swala la madawati. Hata hivyo kasema kuwa swala la madawati lingeweza kushughulikiwa na watumishi wa ngazi za chini na si Rais.

Swala la wabunge wa upinzani kutoka nje ya Bunge amedai kuwa wabunge wa upinzani wana tatizo la kisaikolojia ambalo wengi hatujalijua. Tatizo hilo linatokana na namna naibu spika alivyopatikana akimaanisha mchakato aliyopitia hadi kupatikana. Kwa kauli hii ni dhahiri kuwa wabunge wa upinzani hawajaonewa na naibu spika bali wanatatizo la kisaikolojia hivyo kila maamuzi yanayotolewa kuona kama wanaonewa. Hata hivyo Lowassa anadai anaimani kubwa sana na Job Ndugai spika wa bunge kuwa akirudi kila kitu kitakuwa sawa.

Kuhusu kuhamia upinzani na kukatwa jina lake CCM Mh Lowassa amesema wengi walimlaumu kwa nini alichelewa kuhamia upinzani. Amedai kuna wana ccm wengi walimwambia kuwa kama angelitangaza mapema kuhamia wangelihama naye. Hata hivyo kakanusha kutokufahamu nani alileta wazo la kumwimbia wimbo wa tunaimani na Lowassa. Amedai alishangaa watu kuimba wimbo ule na ulidhihirisha jinsi alivyokuwa anaungwa mkono na wanaccm wenzake. Hata hivyo kakiri kuwa asingelikatwa ndani ya CCM kwa mapenzi ya Mungu Leo angelikuwa ni raisi wa Tanzania.

Mwisho.

Mh Lowassa ameonekana kukataa kujibu maswali Mengi hasa yaliyokuwa yanayomhusu mh Membe ila kamtakia mafanikio mema huko aliko kwa yale anayoyafanya. Amedai bado 2020 atagombea tena na anaamini kuwa atashida. Pia amejivunia kura milioni 6 alizozipata japokuwa anaamini kuwa aliibiwa kura na kadai Ingelikuwa ni nchi Ya Israeli leo hii angelikuwa raisi kwa kuwa nchi hiyo ina idadi watu inayolingana  na  kura alizopata.

................................
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top