Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKAMISHNA WAPYA POLISI WALA KIAPO CHA UADILIFU IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya Makamishna hao kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo.Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wasimamie utekelezaji wa Sheria bila woga na kuahidi kuboresha maslahi ya Jeshi la Polisi nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP)  mara baada ya kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akiwaongoza Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) 35 na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) 23 kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma mara baada yakupandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) wakila Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma mara baada yakupandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) wakifuatilia kwa Makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula Kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Ummaleo Ikulu jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora MheAngellah Kairuki (kushoto) akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi (wa pili kutoka kushoto) Ikulu jijini Dar es salaam mara baada yaNaibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) kula kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma.Wengine niKamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali ProjestRwegasira (wa pili kutoka kushoto)akizungumza jambo naMwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (kushoto) leo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) kula kiapo cha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma.Wengine kulia ni Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Kulia) na Mhe. Hamad Masauni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP) kula Kiapocha Uaminifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo.Kutoka kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju,Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora MheAngellah Kairuki (kushoto),Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama leo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya Naibu Makamishna wa Polisi (DCP) na  Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP).Picha/A.Msigwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top