Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKONGORO NYERERE ANUSURIKA KWENYE AJALI MBAYA

Babati. Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere amenusurika katika ajali baada ya gari lake kuwagonga ng’ombe saba kwenye eneo la Makatanini, Babati mkoani Manyara.

Mtoto huyo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa anatoka Dodoma kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM uliomchagua Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama hicho kwenda Arusha.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Francis Massawe amesema ajali hiyo ilitokea saa 1 usiku jana na kuwaua ng’ombe saba na kondoo mmoja.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo haikuwa na madhara ya binadamu, ni mifugo hiyo kuvushwa barabara sehemu isiyo na kivuko rasmi cha mifugo na katika tukio hilo. Mchungaji wa mifugo hiyo, William German alikimbia baada ya ajali hiyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top