Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKUU WA WILAYA TUNDURU, JUMA HOMERA ASHIRIKI KAMPENI YA KULINDA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera, akiandika Daftari la Wageni katika kijiji cha Misechela, kata ya Misechela.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera, ashiriki Kampeni ya Linda Afya ya Mama na Watoto, yenye kauli mbiu ya "Afya Yako, Furaha Yako".

Kampeni imefanyika katika kata ya Misechela Kijiji cha Misechela yenye Jumla ya Wakazi 2,  524, wanaume 1, 229 na wanawake 1, 295.              

Mradi huu wa "Mpango wa Uboreshaji Afya ya Akina Mama na Watoto" umeasisiwa na Kanisa ya Anglikana  chini ya Ufadhili wa Serikali ya Kanada.

Lengo la Mradi ni kupunguza Vifo vya akina Mama na Watoto chini ya miaka 5, katika eneo la Mradi (Masasi na Tunduru).

Mradi ina hudumia Wilaya mbili, Masasi na Tunduru,  Masasi kata 1 na Tunduru kata 14.

Akizungumza na Wananchi, Mhe. Juma Homera ameagiza Wananchi wafanye kazi kwa bidii na Serikali  inawaunga mkono.                    

 Aidha, aliwaagiza Vijana na akina Mama wajiunge katika Makundi ili waweze kushirikiana kujenga Taifa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top